MTEULE WA UDIWANI VITI MAALUM CHEDEMA - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

DOWNLOAD AJIRA DAILY HAPA

Monday, 26 February 2018

MTEULE WA UDIWANI VITI MAALUM CHEDEMAKwa kuzingatia matakwa ya kifungu cha 86A cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292, Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika Kikao chake cha tarehe 23 Februari, 2018, imemteua Ndugu JANE JAPHALY JOJO kuwa Diwani wa Viti Maalum katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Uteuzi huu umefanyika baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa ambaye kwa mujibu wa kifungu cha 13 (1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292, aliitaarifu Tume ya Taifa ya Uchaguzi uwepo wa nafasi hiyo wazi baada ya kifo cha aliyekuwa Diwani wa Viti Maalum kupitia CHADEMA Ndugu Ester L. Mpwiza.

Tume baada ya kupokea Taarifa hiyo, ilikifahamisha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ambacho kiliwasilisha jina la anayependekezwa kuteuliwa kuwa Diwani wa Viti Maalum kutoka katika orodha ya majina yaliyowasilishwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi mwaka 2015.

Imetolewa leo Jumatatu, tarehe 26 Februari, 2018 na:
Kailima, R. K
MKURUGENZI WA UCHAGUZI


EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ