MATUKIO KWA PICHA NAMNA MWILI WA AKWILIN ULIVYOWASILI KWAO ROMBO - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Friday, 23 February 2018

MATUKIO KWA PICHA NAMNA MWILI WA AKWILIN ULIVYOWASILI KWAO ROMBO

Image result for AKWILIN AKWILIN
Ungana na Edusportstz kupata updates za matukio yanayojili katika shughuli za kuupumzisha mwili wa aliyekuwa mwanafunzi wa NIT Akwilin Akwilin
Wanafunzi ambao alikuwa akisoma nao marehemu Chuo cha NIT wakiwa msibani hapo. Wa kwanza kushoto ni mshauri wa wanafunzi, Paulina Tarazo, Agripina Joseph, Beatrice Charles na Komba Anthony wakiwawakilisha wenzao.

MWILI wa aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji cha Taifa (NIT), Akwilina Akwilini umewasili nyumbani kwao Rombo-Mashati mkoani Kilimanjaro leo Alhamisi, Feb. 23, 2018 majira ya saa 1: 45 asubuhi kwa ajili ya mazishi.


Hali ilivyo nyumbani kwa marehemu.Akiongoza msafara wa waombolezaji waliopeleka mwili huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo na Mkuu wa Chuo cha NIT, Prof. Zakaria Mganilwa wamekabidhi mwili huo kwa familia.


Mwili wa marehemu ukiwasili nyumbani hapo.

Kwa mujibu wa ndugu wa marehemu, shughuli ya kuaga mwili wa marehemu itaanza saa 5:00 asubuhi ambapo mwili utapelekwa kanisani kwa ajili ya ibada ya kuagwa na mazishi yatafuata.


Rafiki wa marehemu wakiwa msibani hapo.Aidha, kwa sasa wanaosubiriwa ili kuendelea na shughuli hiyo ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Ndalichako, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira, makatibu wakuu na manaibu makatibu wakuu, Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini na viongozi wengine.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo akizungumza na waombolezaji wengine.Akwilina aliagwa jana Alhamisi katika viwanja vya NIT vilivyopo Mabibo, Dar es Salaam na kusafirishwa kwenda kijini kwao.


Mwili ukiwasili.


Mwanafunzi huyo alifariki dunia Februari 16, 2018 baada ya kupigwa risasi kichwani akiwa kwenye daladala wakati polisi wakiwatawanya waandamanaji ambao ni wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).


Akwilapo akikabidhi mwili.
Waombolezaji wakikusanyika nyumbani kwao marehemu.
Waombolezaji wakiwa wenye huzuni msibani hapo.
Mwili ukiwasili nyumbani.
Kaburi ambamo atazikwa marehemu.
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ