MATOKEO YA UCHAGUZI WA UBUNGE JIMBO LA KINONDONI NA SIHA - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Sunday, 18 February 2018

MATOKEO YA UCHAGUZI WA UBUNGE JIMBO LA KINONDONI NA SIHA


Image result for tume ya uchaguzi

Kilimanjaro. Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeibuka kidedea katika uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Siha mkoani Kilimanjaro baada ya Tume ya Uchaguzi (Nec), kumtangaza Dk Godwin Mollel kuwa mshindi wa kiti hicho.


Nec imemtangaza rasmi Dk Mollel kuwa mshindi wa uchaguzi huo baada ya kupata kura 25,611 huku akiwaacha mbali wapinzani wake, Elvis Mosi wa Chadema, Elvis Mosi aliyepata kura 5,905 na mgombea wa CUF, Tumsifueli Mwanri aliyepata kura 274 huku Mdoe Azaria wa Sau akiambulia kura 170.

Kwa upande wa Jimbo la Kinondoni jijini Dar es Salaam, hadi saa saba usiku shughuli ya majumuisho ya kura ilikuwa inaendelea lakini matokeo ya awali yaliyobandikwa na wasimamizi wasaidizi katika vituo mbalimbali vya kupigia kura, yanaonyesha kuwa mgombea wa CCM, Maulid Mtulia anaendelea kuongoza.

Mtulia anafuatiwa na mgombea wa Chadema, Salum Mwalimu pamoja na mgombea wa Cuf, Rajab Juma akifuatia kwa tofauti ya kura nyingi.Mgombea Ubunge Jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Maulid Mtulia ameshinda Uchaguzi mdogo uliofanyika jana. Maulid Mtulia Amepata kura 30, 247 dhidi ya Mgombea wa Chadema Aliyepata kura 12, 353.


Elimu YetuEDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati. Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
EDUSPORTSTZ