KIMBEMBE; MBWA AGEUKA BINADAMU WILAYANI MBOZI - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Saturday, 24 February 2018

KIMBEMBE; MBWA AGEUKA BINADAMU WILAYANI MBOZIWananchi wa kijiji cha Mpanda Kata ya Nyimbili wilayani Mbozi mkoani Songwe wameshikwa na taharuki baada ya mbwa aliyewasumbua kwa siku nyingi kwa matukio ya uhalifu hasa kwa kukamata kuku kijijini hapo kugeuka na kuwa binadamu na kuanza kuongea.


Afisa Mtendaji wa kijiji hicho amethibitisha tukio hilo kutokea na kuongeza kuwa wamekumbwa natahauki kubwa kuona kitu cha ajabu binadamu kujibadilisha kuwa mbwa na kuanza kufanya uhalifu kitu ambacho kimewashitua wengi. Inadaiwa mbwa huyo kwa siku alikuwa anakamata kuku kuanzia watatu mpaka wa tano.

Mmoja wa wamashuhuda wa tukio hilo alisimulia kuwa "Kuku walianza kupotea muda mrefu kwa hiyo tulichukua jukumu la kumtaarifa Afisa Mtendaji kwamba kuna mbwa amemaliza kuku za wananchi kwenye kitongoji cha Mpanda kati kwa hiyo baada ya hapo tumeamua kuamka na kuanza kufukuzana na huyo mbwa, tulianza kufukuzana naye kuanzia saa kumi na mbili na kufika saa nne ya asubuhi wakati tunakaribia kumkamata akabadilika na kutokea binadamu" alieleza mwananchi

Afisa Mtendaji aliendelea kusimulia juu ya tukio hilo na kusema baada ya mbwa yule kubadilika na kuwa binadamu alianza kuongea akiwaomba wananchi wamuue na kukiri kuwa yeye ni mchawi na alitumwa.

"Baada ya hapo alijitambulisha anaitwa Happy Victor akaomba tusimrudishe kwao Ilemi bali tumuue na kusema kuwa mtoto wake anatuachia tumle sisi tukasema hapana hatuwezi kukuuwa ila tunakuomba utupe maelezo huku Mbozi umekujaje akasema huku nimekuja kuna mtu amenileta ila mama yangu ni mshirikina alichomewa nyumba kule Ilemi kwa hiyo mimi ni yule mbwa ambaye alipotea kule Ilemi aliyekuwa anatuhumiwa kwamba anakichaa. Sisi tukamsihi kwamba wewe basi sisi tunakuomba hizo nguo vaa akasema nikivaa hizi nguo nitabadilika kuwa mbwa yule wa kichaa" alisema Afisa Mtendaji

Kwa upande wake Afisa Tarafa ya Vwawa Haji Hamisi Ibrahamu amewataka wananchi kuachana na mambo ya kishirikina ambapo amewataka wazee wa mila na wachungaji wakemee tukio hilo na kusema kuwa mtu huyo wao watamfikisha kwenye vyombo vya sheria kwa kufanya uhalifu.


6
Shares


EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.