SHUHUDIA UZURI WA KIVUTIO CHA IRENTE VIEW POINT MKOANI TANGA - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

Friday, 9 February 2018

SHUHUDIA UZURI WA KIVUTIO CHA IRENTE VIEW POINT MKOANI TANGAIrente View Point inapatikana katika kijiji cha Irente kilichopo wilayani lushoto mkoani Tanga, eneo hili liligunduliwa na wazee wa kale ambao walikuwa wakifika hapo kwa ajili ya kuomba na kufanya matambiko na wengine walikuwa wakifika katika eneo hilo kwaajili ya kufanya ibada hasa wakati wa sikukuu za ChristmasEneo hili lina urefu wa Mita 1500 kutoka usawa wa Bahari , ukiwa juu unaweza kuona maeneo mbalimbali vizuri bila usumbufu wowote, pia watalii wengi wamekuwa wakifika eneo hilo kutokana na hali ya hewa kuwa nzuri, kuona Mandhari nzuri hasa wakati wa asubuhi na jioni.


Jinsi ya kufikia ikiwa unatokea upande wowote, fika hadi Mombo, panda daladala Tsh 3,000 mpaka Lushoto mjini baada ya hapo unaweza panda Boda boda Tsh 3,000 au ukachukua Tax Tsh 10,000 , kiingilio ni Tsh 2,000.

Hapa ndipo kileleni na Mwonekano wa Irente


Hii ni Miamba mikubwa iliyopo Irente na moja ya kivutio kikubwa katika eneo hili kwa upande kwa Kushoto.

Eneo hili wakazi wa Irente wanaliita Pango ambapo watu wengi wanapenda kupigia picha

Hii ni njia ya kuelekea Pangoni


Ukiwa Juu ndani ya Pango utaona hivi
Mmoja wa walinzi akiandika akiwakatia risiti wageni mbalimbali waliotembelea eneo hilo.

Watu wengi wamekuwa na utaratibu wa kukalili kuwa wanapoambiwa kwenda kufanya utalii basi mawazo yanahamia katika hifadhi za taifa au Fukwe za Bahari, wakati kuna utalii wa kupanda milima,utalii wa uwindaji utalii wa picha, utalii wa kiutamaduni,Utalii wa Ikolojia,utalii wa fukwe,Michezo ya kwenye maji, utalii wa mali kale,utalii wa mikutano,utalii wa matibabu,utalii wa mashambani na utalii wa jiji.
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au
kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.

BOFYA HAPA KUJIUNGA NA INNOVATION FURSA CHALLENGE

http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji

Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno


EDUSPORTSTZ