BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Tuesday, 6 February 2018

HAYA HAPA MADARAKA YA RAIS


Waziri wa katiba na sheria Profesa. Palamagamba Kabudi amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli ana mamlaka yote ya kutoa maagizo kwa Mawaziri ambao wapo ndani ya serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.Waziri Kabudi ametoa ufafanuzi huo leo (Jumanne) katika mkutano wa 10 kikao cha sita cha Bunge kinachoendelea mjini Dodoma wakati alipokuwa akijibu swali la nyongeza kutoka kwa Mbunge Juma kombo Hamadi alipotaka kufahamu Rais Magufuli ana mamlaka gani kikatiba ya kutoa maagizo kwa Waziri aliyepo katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

"Rais wa Muungano wa Tanzania anayo mamlaka ya mambo yote yanayohusu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama nchi huru", amesema Prof. Palamagamba.

Pamoja na hayo, Prof. Palamagamba ameendelea kufafanua baadhi ya mambo kuwa "katika masuala yote yanayohusu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mkuu wa nchi ni mmoja tu tena ambaye ni Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na yeye peke yake ndio Amri Jeshi. Hakuna mtu mwingine yeyote wa kuyaamuru majeshi ya Tanzania isipokuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa sababu yeye ndio kiongozi mkuu wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania".

Kwa upande mwingine, Prof. Palamagamba amesema Rais wa Zanzibar ni wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar mwenye heshima na hadhi ya urais kwa mambo yote yasiyokuwa ya Muungano yanayohusu Zanzibar ambapo pia ni Mjumbe wa Baraza la Mawaziri la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa nafasi yake hiyo.
NDG MSOMAJI WA EDUSPORTSTZ UNAKUMBUSHWA KUSUBSCRIBE NA KUFOLLOW WEB YETU PAMOJA NA MITANDAO YETU YA KIJAMII CHINI YA POSITI HII ILI KUTUMIWA UPDATES ZOTE ZA AJIRA, MICHEZO, HABARI, SCHOLARSHIPS PAMOJA NA MASTORI YA MASTAA NA VIONGOZI MBALIMBALI. EDUSPOTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI.
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati. BOFYA HAPA KUJIUNGA NA INNOVATION FURSA CHALLENGE http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
UNGANA NASI KUPITIA LIKI HIZI ILI KUTUMIWA HABARI POPOTE ULIPO

EDUSPORTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI

WEKA EMAIL YAKO:


Delivered by EDUSPOTSTZ
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
EDUSPORTSTZ

No comments:

Post a Comment