BWENI LATEKETEA MOTO MKOANI MBEYA - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

Friday, 16 February 2018

BWENI LATEKETEA MOTO MKOANI MBEYA


Bweni la wasichana wa shule ya sekondari Kipoke mkoani Mbeya limeteketea kwa moto na kusababisha uharibifu mkubwa huku wanafunzi wawili wakijeruhiwa.

Hayo yamethibitishwa na Mkurugenzi wa shule hiyo Gervas Mwanyila wakati alipokuwa anazungumza na mwandishi wa habari wa EATV na kusema ni kweli tukio hilo limetokea katika shule yao japokuwa mpaka sasa hawajafahamu chanzo chake.

"Ni bweni la wasichana kidato cha pili limeungua moto ambapo mpaka sasa hatujajua chanzo chake kama ni umeme au ni wanafunzi wenyewe tumeshindwa kufahamu. Tumefanya jitihada za kunusuru vitu vya wanafunzi na wao wenyewe lakini tumefanikiwa kwa kiasi kidogo kutokana na baadhi ya vitu ikiwemo magodoro na vitanda 68 kuteketea na moto", amesema Mwanyila.

Pamoja na hayo, Mwanyila ameendelea kwa kusema "ni vijana watano pekee waliojeruhiwa kidogo na moto huo baada ya wao kusaidia kukata bati ili moto usiweze kuenea katika maeneo mengine ya bweni".

Kwa upande mwingine, Mwanyila amesema bado hawajaweza kujuwa tathimini kamili ya mali za shule zilizoweza kuteketea na moto kutokana bado hawatulia tokea ajali hiyo ya moto ilipoanza.

Elimu Yetu

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati. Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mnoEdusportstz↑ Grab this Headline Animator