BALOZI MBOWETO NA DK. SLAA WAMUAGA MAKAMU WA RAIS OFISINI KWAKE LEO JUMAMOSI - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Saturday, 17 February 2018

BALOZI MBOWETO NA DK. SLAA WAMUAGA MAKAMU WA RAIS OFISINI KWAKE LEO JUMAMOSIBalozi wa Tanzania nchini Nigeria Mhe. Muhidin Ally Mboweto pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Sweden Mhe. Wilbrod Peter Slaa leo wamekutana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye makazi yake Oysterbay, jijini Dar es Salaam kwa lengo la kumuaga tayari kwenda kwenye vituo vyao vipya vya kazi.

Mabalozi hao waliapishwa jana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar Es Salaam .

Makamu wa Rais aliwatakia safari njema huko waendapo kwenye vituo vipya vya kazi ambapo aliwasihi kwenda kufanya kazi kwa moyo mmoja na kuzingatia maelekezo ya Mhe. Rais

“Hakikisheni mnaitangaza nchi yetu vizuri na kuwashawishi wawekezaji ili waweze kuja kwa wingi, nchi yetu ina fursa za kutosha” alisema Makamu wa Rais.

Kwa upande wao Mabalozi hao walimuahidi Makamu wa Rais kuiwakilisha nchi vizuri na kufanya kazi kizalendo.

Elimu Yetu
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati. Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
EDUSPORTSTZ