BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Monday, 12 February 2018

BADNEWS. AJARI YA GARI YAWAUA ABIRIA WA TANO MKOANI TANGA


Kwa mujibu wa habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Leo Rwegasira, ajali hiyo imetokea leo Februari 12 saa tano.Burhani Yakub na Rajab Athumani Mwananchi


Handeni. Abiria watano wamekufa papo hapo akiwamo dereva na wengine sita kujeruhiwa baada ya basi la abiria kugongana uso kwa uso na gari ndogo katika kitongoji cha Mwituni Kijiji cha Kabuku wilayani hapa.

Kwa mujibu wa habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Leo Rwegasira, ajali hiyo imetokea leo Februari 12 saa tano.

Kamanda huyo amesema kwamba basi hilo lilikuwa linatokea Lushoto kuelekea Jijini Dar es salaam na na jingine lilitokea Kijiji cha Mkata.

Waliokufa katika ajali hiyo kwa mujibu wa Kaimu Kamanda Rwegasira ni dereva wa Hiace, aliyetambulika kwa jina moja la Shaaban huku wengine wanne wakiwa bado hawajatambuliwa majina yao lakini wote ni wanaume.

“Majeruhi ambao tumewakimbiza hospitali wapo sita akiwamo dereva wa basi kubwa, Khalifa Omar (33) aliyepata majeraha sehemu mbalimbali za mwili wake na wengine majina yao yatatolewa baada ya madaktari kuwapa huduma ya tiba ya awali,” amesema Rwegasira.

Ali Juma ambaye alishuhudia ajali hiyo na kushiriki uokoaji wa majeruhi amesema alishtuka baada ya kusikia kishindo ndipo aliposogea akaona magari hayo yakiwa yamegongana huku abiria wakiomba kupewa msaada.

Kaimu Kamanda huyo amesema Jeshi la Polisi linafuatilia kujua chanzo cha ajali hiyo na kuwaonya madereva wawapo barabarani kufuata sheria za barabarani.
Elimu Yetu
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati. Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
EDUSPORTSTZ

No comments:

Post a Comment