ALIYOYASEMA MBOWE LEO AKIWA NA WAANDISHI WA HABARI - EDUSPORTSTZ

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Tuesday, 27 February 2018

ALIYOYASEMA MBOWE LEO AKIWA NA WAANDISHI WA HABARI


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia kwa Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe kimeongea na waandishi wa habari leo katika Makao makuu yao.

Mbowe amesema Usalama wa Taifa wanaratibu mikakati ya kuwabambikizia kesi wana CHADEMA na wao wamejipanga kutokana na huo mkakati. Amemwambia Rais Magufuli kuwa wapo tayari kwa lolote maana wanapigania demokrasia.

Mbowe amesema Mkoa wa Morogoro unaongoza kwa kuwabambikizia kesi viongozi wao. Lakini hata kwa mauaji, Mkoa huo unaongoza maana kuna historia ya watu wa CHADEMA kuuawa.

Amemuhusisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Bwana Amosi Makala kwenye kuratibu kesi ya Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi(Sugu).Amesema hukumu ilifahamika na ilipangwa Hotelini, wote walifahamu na Amosi Makala anajua hilo


Aliongeza kwa kusema “CCM kama wanataka kurudisha uhalali wao wa uongozi waseme na wananchi watawaelewa na sio kutumia bunduki kukatisha uhai wa watu. Halafu tumeshaanza kuzoea kuuwawa, hili jambo si zuri maana tunakoelekea ni kutaka kuua upinzani”
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ

No comments:

Post a Comment