BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Monday, 12 February 2018

BADNEWS; NDEGE ILIYO KUWA NA ABIRIA 71 YAPATA AJALI


Ndege iliyotoweka ya An-148 ni sawa na iliyo kwenyr picha hii

Ndege ya Urusi iliyokuwa imebeba abiria 71 na mhudumu imeanguka baada ya kupoteza mawasiliano ilipokuwa ikiondoka uwanja wa mjini moscow.

Ndege hiyo ya shirika la Saratov ya An-148, ilikuwa safarini kwenda mji wa Orsk wakati ilipoteza mawasiliano.

Huduma za dharura ziliambia vyombo vya habari kuwa ndege hiyo ilianguka na hakuna uwezekano wa kuwapata manusura

Inaripotiwa kuanguka karibu na Argunovo kilomita 80 kusini mashariki mwa Moscow.

Kulingana na shirika lingine na habari ndege hiyo ilipotea kutoka mitambo ya rada dakika mbili baada ya kuondoka uwanja wa Domodedovo.

Mabaki ya ndege hiyo na miili ilipatikana imetapakaa eneo kubwa. Kifaa kimoja cha kurekodi safari za ndege kimepatikana.

Rais Vladimir Putin ametuma rambi rambi zake kwa familia za waathiriwa na kutaka uchunguzi kufaywa kuhusu kilochosabaisha ajali hiyo.
Elimu Yetu
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati. Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
EDUSPORTSTZ

No comments:

Post a Comment