AGIZO LA MKUU WA WILAYA TEMEKE KWA BODABODA - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

DOWNLOAD AJIRA DAILY HAPA

Sunday, 25 February 2018

AGIZO LA MKUU WA WILAYA TEMEKE KWA BODABODA


MKUU wa Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam, Felix Lyaniva amewataka madereva wa pikipiki na Bajaj kuwa makini na kuzingatia sheria za usalama barabarani ikiwemo kuvaa kofia ngumu na viatu wakati wanapoendesha vyombo vya moto.

Amesema lengo ni kuepuka ajali zinazosababishwa na madereva wazembe na kuwataka kufanya kazi kwa kuzingatia sheria zilizopo.

Lyaniva ameyasema hayo jana , wakati wa utambulishaji rasmi wa mfumo wa namba utakaowatambulisha madereva pikipiki na bajaji katika vituo vyao mbalimbali katika katika Kata ya Kibondemaji, Mbagala Jijini Dar es salaamu uliofadhiliwa na Diwani wa Kata hiyo Abdallah.

Diwani huyo ameshirikiana na Kampuni ya Tanzania Motorcycle and Bajaji Association (TAMOBA) kwa ajili ya kuzisajili Pikipiki na Bajaji katika mfumo wa GPS utakaowawezesha kujua Pikipiki iliyoibiwa ipo eneo gani na kuweza kupatikana kwa haraka zaidi.Akizungumza zaidi Lyaniva amewapiga marufuku mgambo wa wilaya hiyo kutokamata pikipiki na Bajaj kwani wengi wao wamekuwa wakikamata pikipiki hizo bila ya kuzingatia sheria.

Amesena kazi ya kukamata bodaboda itafanywa na askari wenye weledi na wenye kujua sheria za usalama barabarani.Lyaniva pia amewapongeza TAMOBA kwa kuwafikia madereva bodaboda na bajaj kwani walikuwa na wasiwasi wa kuibiwa vyombo vyao na kuporwa na majambazi.

Ameongeza Diwani huyo ameleta maendeleo makubwa na mazuri katika Kata hiyo na pia TAMOBA imeleta usalama mzuri kabisa wa kisasa kwa kuwa madereva hao watafanya kazi zao wakiwa hawana wasiwasi wa kuibiwa Pikipiki zao na mali zao wawapo katika majukumu yao hayo pamoja na abiria wao.EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ