UNHCR YAPINGA VIKALI KUHUSU WAHAMIAJI KUTOKA BARANI AFRIKA - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Thursday, 11 January 2018

UNHCR YAPINGA VIKALI KUHUSU WAHAMIAJI KUTOKA BARANI AFRIKAafrika
Israel imetoa ilani ya siku tisini kwa maelfu ya wahamiaji kutoka Afrika

Umoja wa Mataifa umelaani mpango wa Israel wa kuwaondoa wakimbizi kama usioeleweka na si salama, unaokusudia kuwafukuza maelefu ya wakimbizi Waafrika nchini humo.


Shabaha ya mpango wa Israeli inawahusu wakimbizi 38,000, wengi wao ni Waeritrea na Wasudan. Yasemwa akufukuzaye hakuambii ondoka, muondoko huo umepakawa sukari ya $3,500 na tiketi ya ndege kwa kila mkimbizi. Wakimbizi hao wakikataa, kufikia Machi mwaka huu 2018, watakamatwa.

Shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR liliukosoa vikali mpango huo na kutoa wito kwa Israel isimamishe sera hiyo, kwa sababu haieleweki wala haitekelezwi kwa njia wazi.


Mpaka sasa Israeli haijasema wapi wakimbizi hao wanakwenda. Lakini kwa mujibu wa watetezi nchini Israeli, kuna mapatano baina ya Israel na Uganda na Rwanda kuwapokea wakimbizi hao ilimradi wameridhia.

Ingawa Uganda na Rwanda mara kadhaa zimekanusha kuwepo kwa maafikiano aina hiyo. Watu 80 ambao walihojiwa Roma na UNHCR, walisema walipelekwa kwa ndege hadi Rwanda na $3,500 kila mmoja. Licha ya kuwa waliondoka Rwanda. wakaelekea kaskazini kupitia maeneo ya vita Sudan Kusini, Sudan na Libya, na kuhatarisha maisha kuvuka Bahari Mediterranean kuingia Italia huku njiani waliteswa na kunyanyaswa.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati. BOFYA HAPA KUJIUNGA NA INNOVATION FURSA CHALLENGE http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
UNGANA NASI KUPITIA LIKI HIZI ILI KUTUMIWA HABARI POPOTE ULIPO

EDUSPORTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI

WEKA EMAIL YAKO:


Delivered by EDUSPOTSTZ
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
EDUSPORTSTZ