UKWELI KUHUSU HALI YA KATIBU MKUU WA CHADEMA HUU HAPA - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

Thursday, 18 January 2018

UKWELI KUHUSU HALI YA KATIBU MKUU WA CHADEMA HUU HAPANDG MSOMAJI WA EDUSPORTSTZ UNAKUMBUSHWA KUSUBSCRIBE NA KUFOLLOW WEB YETU PAMOJA NA MITANDAO YETU YA KIJAMII CHINI YA POSITI HII ILI KUTUMIWA UPDATES ZOTE ZA AJIRA, MICHEZO, HABARI, SCHOLARSHIPS PAMOJA NA MASTORI YA MASTAA NA VIONGOZI MBALIMBALI. EDUSPOTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI.
Chadema Wakanusha Taarifa za Kuugua Ghafla Katibu Mkuu Wao

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimekanusha taarifa zinazosambaa mitandaoni kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, DR.Vincent Mashinji amelazwa katika hospitali ya Amana baada ya kuumwa ghafla.


Akizungumza na mwandishi wa www.eatv.tv Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje- CHADEMA bwana John Mrema amesema kuwa taarifa hizo hazina ukweli wowote na kudai kuwa Katibu wao ni mzima wa afya na sasa anaendelea na kikao cha Kamati Kuu ya CHADEMA kinachofanyika Bahari Beach jijini Dar es Salaam.

"Tumeiona hiyo taarifa ila si ya kweli na sijui wameitoa wapi kwani Katibu Mkuu ni mzima wa afya njema na hivi naongea na wewe tupo naye kwenye vikao vya Kamati Kuu ya CHADEMA hapa Bahari Beach" alisema Mrema

Mapema leo zimezuka taarifa kuwa kiongozi huyo wa CHADEMA ameugua ghafla na kupelekwa hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam kwa matibabu zaidi na kuwa alitembelewa na Katibu Mkuu wa CUF akiwa hospitali hapo, japo ambalo limepingwa na Bwana Mrema


EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati. BOFYA HAPA KUJIUNGA NA INNOVATION FURSA CHALLENGE http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
UNGANA NASI KUPITIA LIKI HIZI ILI KUTUMIWA HABARI POPOTE ULIPO

EDUSPORTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI

WEKA EMAIL YAKO:


Delivered by EDUSPOTSTZ
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
EDUSPORTSTZ