SERIKALI YAFUNGUKA KUHUSU MADAI YA MELI YATANZANIA KUKAMATWA UGIRIKI - EDUSPORTSTZ | Habari za Ajira, Mapenzi, Michezo, Elimu, Kilimo, Technology, Siasa na Mziki,

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Friday, 12 January 2018

SERIKALI YAFUNGUKA KUHUSU MADAI YA MELI YATANZANIA KUKAMATWA UGIRIKISERIKALI imesema inachunguza taarifa za meli iliyokamatwa nchini Ugiriki ikiwa na bendera ya Tanzania ikipeleka vilipuzi Libya.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Susan Kolimba, akizungumza na Nipashe jana kuhusu tukio hilo, alisema wanafuatilia kwa kina ili kupata ukweli wake.

“Kwa sasa ni kwamba jambo hilo tunalifuatilia ili kujua habari hizo kama zina ukweli na tutakapopata taarifa tutawajulisha, bado tunafuatilia,” alisema Kolimba.

Jana, Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) ilieleza kuwa maofisa wa Ugiriki wanaofanya doria baharini wameizuia meli hiyo iliyokuwa inapeperusha bendera ya Tanzania ikiwa imebeba vilipuzi.

Taarifa hiyo ya BBC ilieleza kuwa meli hiyo inadaiwa kusafirisha vilipuzi hivyo kutoka Uturuki kwenda Libya, kinyume cha sheria iliyowekwa ya kutosafirisha silaha kwenda Libya.

Iliongeza kuwa maofisa hao wameeleza kwamba meli hiyo ilikuwa imebeba kreti 29 zilizojaa vilipuzi pamoja na kemikali zinazotumiwa kuunda vilipuzi.

"Maofisa wa kushika doria baharini wamezima bomu lililokuwa linasafiri," ofisa mkuu wa walinzi hao wa Ugiriki, Yiannis Sotiriou alikaririwa na BBC jana.

Taarifa ya BBC ilieleza kuwa Wizara ya Safari za Baharini ilisema meli hiyo ilisimamishwa ikiwa katika kisiwa cha Crete kusini mwa Ugiriki baada ya maofisa kupatiwa taarifa na ilisindikizwa hadi katika bandari ya kisiwa hicho na kufanyiwa ukaguzi.

Sotiriou alikaririwa katika taarifa hiyo akieleza kuwa meli hiyo ambayo ilinaswa Jumamosi ilikuwa pia na kasoro nyingi na haikufaa kuwa baharini.

"Ingesababisha madhara makubwa sana kwa watu na mazingira pia," alikaririwa katika ripoti hiyo ya BBC.

Ilielezwa zaidi katika ripoti hiyo kuwa nahodha wa meli hiyo ambaye alifahamika kwa jina moja la Andromeda, alidai meli hiyo ilikuwa inasafiri kuelekea Djibouti lakini baadaye ikabainika kwamba ilikuwa inasafiri kuelekea mji wa bandarini wa Misrata nchini Libya.

Kwa mujibu wa ripoti ya BBC, mabaharia wanane ambao ni raia wa India, Ukraine na Albania waliokuwa kwenye meli hiyo, walitarajiwa kufikishwa mbele ya mwendesha mashtaka jana
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati. BOFYA HAPA KUJIUNGA NA INNOVATION FURSA CHALLENGE http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
UNGANA NASI KUPITIA LIKI HIZI ILI KUTUMIWA HABARI POPOTE ULIPO

EDUSPORTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI

WEKA EMAIL YAKO:


Delivered by EDUSPOTSTZ
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
EDUSPORTSTZ

No comments:

Post a Comment