SABABU ZA MBUNGE MCHUNGAJI MSIGWA KUKAMATWA HIZI HAPA - EDUSPORTSTZ

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Tuesday, 23 January 2018

SABABU ZA MBUNGE MCHUNGAJI MSIGWA KUKAMATWA HIZI HAPAKamanda wa polisi mkoa wa Iringa, (RPC) Julius Mjengi amefunguka na kuweka wazi sababu zilizopelekea kumkamata Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa na kudai kuwa walimkamata wakimtuhumu kuratibu kuchoma na kubomoa nyumba.
Mjengi amesema hayo leo Januari 23, 2018 wakati akiongea na www.eatv.tvna kudai kuwa Mbunge huyo jana alipokamatwa alihojiwa na baadaye aliachiwa kwa dhamana hivyo yupo huru kwa dhamana toka jana majira ya saa tano usiku.

"Jana Msigwa alijisalimisha baada ya kusikia tunamtafuta hivyo tulimuhoji na usiku alipata dhamana, hivyo sisi tulikuwa tunamtafuta kwa tuhuma za kuratibu matukio mawili ya uhalifu hapa Iringa Mjini ambapo kuna nyumba ya diwani mmoja ambaye alijiuzulu na kuhama CHADEMA na kuhamia CCM nyumba yake pagale lilibomolewa"

Kamanda aliendelea kusema kuwa

"Lakini pia usiku wa kuamia tarehe 17 kuna nyumba moja Kihesa ilichomwa moto ikateketea na ndani mle katika wapangaji mmoja alikuwa ni Katibu wa UVCCM Wilaya ya Iringa Mjini kwa hiyo Msigwa ana tuhuma za kuratibu matukio haya, kwa hiyo tulimuhoji na kudhamini ila tunaendela naye" alisisitiza Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa, (RPC) Julius Mjengi
NDG MSOMAJI WA EDUSPORTSTZ UNAKUMBUSHWA KUSUBSCRIBE NA KUFOLLOW WEB YETU PAMOJA NA MITANDAO YETU YA KIJAMII CHINI YA POSITI HII ILI KUTUMIWA UPDATES ZOTE ZA AJIRA, MICHEZO, HABARI, SCHOLARSHIPS PAMOJA NA MASTORI YA MASTAA NA VIONGOZI MBALIMBALI. EDUSPOTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI.
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati. BOFYA HAPA KUJIUNGA NA INNOVATION FURSA CHALLENGE http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
UNGANA NASI KUPITIA LIKI HIZI ILI KUTUMIWA HABARI POPOTE ULIPO

EDUSPORTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI

WEKA EMAIL YAKO:


Delivered by EDUSPOTSTZ
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
EDUSPORTSTZ

No comments:

Post a Comment