BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Tuesday, 30 January 2018

RAILA ODINGA AJIAPISHA KUWA RAIS WA KENYA,FUATILIA MATUKIO YALIYOJILI

Upinzani washerehekea kuapishwa kwa Odinga
Shangwe na nderemo zinaendelea katika maeneo ya Kisii na Homa Bay, magharibi mwa Kenya ambayo ni maeneo ya ngome za upinzani

Wakazi mjini Kisii washerehekea baada ya Raila Odinga kulishwa kiapo


Wakazi wa Homa Bay washerehekea kiapo cha Raila #NASA Oath Day

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga ameapishwa kuwa rais wa wananchi.

Kiapo hicho alilishwa na mbunge wa Ruaraka TJ Kajwang.

Hatahivyo wakuu wa chama hicho akiwemo Kalonzo Musyoka, Musalia Mudavadi na Moses Wetangula hawakuwepo wakati wa kiapo hicho kilichochukuliwa katika eneo la Uhuru Park
Getty ImagesRaila Odinga na naibu wake Kalonzo Musyoka katika picha ya awali

Raila aondoka uwanja wa Uhuru Park

Punde tu alipofika na 'kula kiapo' Raila Odinga ameondoka.

Wengi wamekuwa wakisubiri kwa hamu na ghamu, bila kutegemea kwamba atachukua muda mfupi hivyo.

Awali Raila Odinga aliiambia kituo cha habari cha KTN kwamba shughuli hio ' si mapinduzi ya serikali'

Odinga akula kiapo uwanja wa Uhuru Park

Raila Odinga amefika katika pamoja na viongozi kadha wakuu wa NASA na kujiapisha akishika Biblia.

Amewaambia kuwa mgombea mwenza wake Kalonzo Musyoka wa chama cha Wiper ataapishwa baadaye.

Viongozi wengine wenza wa Nasa Moses Wetangula na Musalia Mudavadi pia hawakufika katika wuanja huo.

Bw Odinga amesema leo ni siku ya kihistoria kwa Kenya.

"Hatua ya leo ni kuelekea kutoa udikteta na kuleta demokrasia Kenya"

"Maelekezo mengine mtayapata baadae"
KTN YoutubeRaila 'akula kiapo'

HABARI ZA HIVI PUNDEOdinga aingia uwanjani na kujiapisha kuwa rais wa wananchi

Kiongozi wa upinzani Raila Odinga ameingia Uhuru Park na moja kwa moja akainua Biblia na kula kiapo kama kiongozi wa wananchi wa Kenya.

Wengi wajitokeza kushuhudia Odinga 'akila kiapo'


Baada ya polisi kuondoka uwanja wa Uhuru Park, wafuasi wa upinzani walianza kuingia kwa wingi na kwa sasa maelfu wamo ndani.

Odinga bado anasubiriwa Uhuru Park

Afisa mkuu mtendaji wa muungano wa National Super Alliance (Nasa) Norman Magaya alikuwa amesema Bw Odinga, na viongozi wengine wa muungano huo wangewasili uwanjani katika muda wa dakika 40 hivi.

Sasa hivi ni saa moja inaelekea kupita tangu wakati huo:

NationBreakingNews
✔@NationBreaking


NASA PRINCIPALS to arrive in Uhuru Park in 40 minutes for the swearing-in ceremony, CEO

Odinga: Tunachokifanya si mapinduzi ya serikali

BBC

Bw Raila Odinga amezungumza na kituo cha habari cha KTN kwa njia ya simu ambapo amesisitiza kwamba Rais Uhuru Kenyatta hakuchaguliwa kwa njia halali.

Alipoulizwa anni atamwapisha, amesema: "Ngoja uone” na akasisitiza kwamba wanachokifanya leo kina msingi wake katika sheria na si mapinduzi.

“Hatutambui uchaguzi wa Oktoba 26 (uchaguzi wa marudio ambao Odinga alisusia), zaidi ya asilimia 86 ya Wakenya hawakushiriki. Tuna serikali ambayo si halali ambao inajidai kuwa mamlakani,” amesema.

Kuhusu taarifa kwamba amepokonywa walinzi, amesema: "Walinzi wangu waliondolewa muda mrefu sana uliopita. Najihisi kuwa hatarini ndio lakini watu raia ndio usalama wangu.”

Bw Odinga ameitaka serikali kutotumia nguvu kuusambaratisha mkutano wa leo.

"Wafuasi wangu wamo safarini kuelekea Canaan. Safari yetu ni halisi na haiwezi

NDG MSOMAJI WA EDUSPORTSTZ UNAKUMBUSHWA KUSUBSCRIBE NA KUFOLLOW WEB YETU PAMOJA NA MITANDAO YETU YA KIJAMII CHINI YA POSITI HII ILI KUTUMIWA UPDATES ZOTE ZA AJIRA, MICHEZO, HABARI, SCHOLARSHIPS PAMOJA NA MASTORI YA MASTAA NA VIONGOZI MBALIMBALI. EDUSPOTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI.
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati. BOFYA HAPA KUJIUNGA NA INNOVATION FURSA CHALLENGE http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
UNGANA NASI KUPITIA LIKI HIZI ILI KUTUMIWA HABARI POPOTE ULIPO


EDUSPORTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI

WEKA EMAIL YAKO:


Delivered by EDUSPOTSTZ
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
EDUSPORTSTZ

No comments:

Post a Comment