NYUMBA YA KATIBU WA VIJANA UVCCM YACHOMWA MOTO - EDUSPORTSTZ

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Thursday, 18 January 2018

NYUMBA YA KATIBU WA VIJANA UVCCM YACHOMWA MOTONDG MSOMAJI WA EDUSPORTSTZ UNAKUMBUSHWA KUSUBSCRIBE NA KUFOLLOW WEB YETU PAMOJA NA MITANDAO YETU YA KIJAMII CHINI YA POSITI HII ILI KUTUMIWA UPDATES ZOTE ZA AJIRA, MICHEZO, HABARI, SCHOLARSHIPS PAMOJA NA MASTORI YA MASTAA NA VIONGOZI MBALIMBALI. EDUSPOTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI.

Nyumba ya Katibu wa Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wa Mkoa wa Iringa, Alphonce Muyinga iliyopo maeneo ya Kihesa njiapanda ya Kwabeda imechomwa moto na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo.


Ambapo kikosi cha Zima Moto kilifanikiwa kufika katika nyumba hiyo na kujaribu kuzima moto huo ambao tayari ulikuwa umeshaleta athari ndani ya nyumba hiyo kwa mali mbalimbali zilizokuwepo ndani.


Pia aliyekuwa Diwani wa kata ya Mwangata, Iringa kwa tiketi ya Chadema na baadaye kujiuzulu nafasi yake hiyo, Anjelus Mbogo naye amefanyiwa uharibifu katika nyumba ambayo alikuwa akijenga baada ya watu wasiojulikana kuibomoa nyumba hiyo.


Anjelus amedai kuwa tukio hilo linawezekana kuwa limetokea kutokana na matamko ya uchochezi yaliyotolewa na Mbunge kwa wananchi.


“Kauli ya Mbunge ndiyo inaweza kuwa chanzo cha uchochezi kwa wananchi kuja kubomoa nyumba hizi kwa sababu yeye aliwaambia wananchi kama atajiuzulu wabomoe nyumba yake hata gari yake ichomwe moto nadhani wananchi wakachukua hilo kwani wananchi unapowashawishi ndivyo unavyomuaminisha kuja kufanya hivi huo ndiyo ukweli. Na mimi sisemi mambo mengi kwa kuwa jambo hilo bado linaendelea na upelelezi lakini naamini wameniaminisha kuwa hatabaki mtu” amesema Anjelus Mbogo


Aidha amesema hawezi kuongea mengi zaidi kwani swala hilo linafanyiwa upelelezi kubaini watu hao wasiojulikana.

 EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.

 BOFYA HAPA KUJIUNGA NA INNOVATION FURSA CHALLENGE http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
UNGANA NASI KUPITIA LIKI HIZI ILI KUTUMIWA HABARI POPOTE ULIPO

EDUSPORTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI

WEKA EMAIL YAKO:


Delivered by EDUSPOTSTZ
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
EDUSPORTSTZ

No comments:

Post a Comment