NABII TITO ANA MATATIZO YA AKILI JESHI LA POLISI LATHIBITISHA - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Tuesday, 23 January 2018

NABII TITO ANA MATATIZO YA AKILI JESHI LA POLISI LATHIBITISHA



NDG MSOMAJI WA EDUSPORTSTZ UNAKUMBUSHWA KUSUBSCRIBE NA KUFOLLOW WEB YETU PAMOJA NA MITANDAO YETU YA KIJAMII CHINI YA POSITI HII ILI KUTUMIWA UPDATES ZOTE ZA AJIRA, MICHEZO, HABARI, SCHOLARSHIPS PAMOJA NA MASTORI YA MASTAA NA VIONGOZI MBALIMBALI. EDUSPOTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI.
Onesmo Machija (44) anayejiita ‘nabii’ Tito.

JESHI la Polisi mkoani Dodoma, baada ya kumkamata na kumfanyia mahojiano Onesmo Machija (44) anayejiita ‘nabii’ Tito, kutokana na mahubiri ya kidini anayoyafanya, limesema mtu huyo ana matatizo ya akili.

Akizungumza na wanahabari mjini Dodoma leo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, Gillesi Muroto, amesema mnamo Juni 23, 2014, mtu huyo aliwahi kulazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya matibabu ya akili chini ya daktari aliyejulikana kwa jina moja la William ambapo aliporuhusiwa alitakiwa kurejea hospitalini hapo Julai 9 mwaka huohuo lakini hakurejea.
Nabii Tito Mbaroni, Abainika na Ugonjwa wa Akili

Muroto aliendelea kusema kwamba baada ya hapo, Machija ambaye kanisa lake halijasajiliwa popote, aliibukia mkoani Dodoma katika kijiji cha Nong’ona kilicho karibu na Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) akifanya mahubiri ya kidini yaliyodaiwa kuwa hayakuwa na maadili ya kidini.

Kwa msingi huo, alisema jeshi la polisi limempeleka Hospitali ya Rufaa ya Mirembe iliyoko mkoani Dodoma kwa ajili ya kumpima tena matatizo hayo ya akili na baada ya majibu kutolewa, Dkt. Dixon Philipo aliyemshughulikia alithibitisha kwamba bado ana matatizo hayo.
Pamoja na hayo, Muroto alisema jeshi la polisi mkoani humo bado linaendelea kumshikilia kutokana na matendo yake aliyoyafanya ili kufanya uchunguzi zaidi.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati. BOFYA HAPA KUJIUNGA NA INNOVATION FURSA CHALLENGE http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
UNGANA NASI KUPITIA LIKI HIZI ILI KUTUMIWA HABARI POPOTE ULIPO

EDUSPORTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI

WEKA EMAIL YAKO:


Delivered by EDUSPOTSTZ
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
EDUSPORTSTZ