;
LOWASSA AFUNGUKA WALICHOONGEA NA RAIS MAGUFULI ALIPOMTEMBELEA IKULU - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Monday, 15 January 2018

LOWASSA AFUNGUKA WALICHOONGEA NA RAIS MAGUFULI ALIPOMTEMBELEA IKULU


Lowassa na Magufuli walikutana Ikulu kwa mara ya kwanza baada ya uchaguzi wa 2015

Mjumbe wa kamati kuu ya chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, CHADEMA, Edward Lowassa amefichua kuwa Rais John Magufuli alimuomba arejee chama tawala cha CCM wakati wa mazungumzo yao juma lililopita.

Katika taarifa iliyotolewa kwa waandishi wa habari na Chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, Lowassa ameeleza: "Ujumbe wa Rais Magufuli ulikuwa kunishawishi kutaka nirejee CCM, suala ambalo sikukubaliana nalo na nilimueleza Rais ya kwamba uamuzi wangu wa kukihama chama hicho na kujiunga na CHADEMA haukuwa wa kubahatisha".

Wiki iliopita, kiongozi huyo wa upinzani nchini Tanzania, ambaye pia ni Waziri mkuu wa zamani, alikutana na Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli Ikulu na kumsifu sana kwa kazi anayoifanya.

Ni hatua ambayo iliwashangaza wengi kwani si kawaida kwa kiongozi huyo kumsifu Rais Magufuli kwani kwa muda amekuwa akikosoa utawala wake.

Bw Lowassa aliwania urais kupitia chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 2015 lakini akashindwa na Dkt Magufuli aliyewania kupitia Chama cha Mapinduzi.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati. BOFYA HAPA KUJIUNGA NA INNOVATION FURSA CHALLENGE http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
UNGANA NASI KUPITIA LIKI HIZI ILI KUTUMIWA HABARI POPOTE ULIPO

EDUSPORTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI

WEKA EMAIL YAKO:


Delivered by EDUSPOTSTZ
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
EDUSPORTSTZ

Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB