KIONGOZI MWNGINE WA UPINZANI ATAMANI KUONANA NA RAIS MAGUFULI - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Friday, 12 January 2018

KIONGOZI MWNGINE WA UPINZANI ATAMANI KUONANA NA RAIS MAGUFULI


Hashim Rungwe Naye Ataka Kuonana na Rais Ikulu
Mwenyekiti Chama cha Chaumma, Hashim Rungwe amesema anatamani kwenda Ikulu kuonana na Rais John Magufuli ili kumweleza mambo ambayo yatawezesha kusaidia kuleta mabadiliko katika utawala wake.

Akizungumza na Mwananchi leo Ijumaa Januari 12, 2018, Rungwe amesema kila mtu anatamani kuonana na Rais Magufuli lakini nafasi hiyo imekuwa haipatikani.

Rungwe anatoa kauli hiyo ikiwa imepita siku tatu tangu waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa alipofanya ziara Ikulu na kuzungumza na Rais Magufuli.

“Hata mimi nataka kuonana na Rais, nimekuwa natamani sana lakini hatupati nafasi hiyo, nikikutana naye tutazungumza mambo mengi, ambayo yatamsaidia yeye mwenyewe katika uongozi wake,” amesema Rungwe na kuongeza;

“Sisi upinzani tulikuwa tunasema hatutaki mafisadi, hatutaki wabidhirifu au tunapiga kelele dawa hakuna hospitalini kwa hiyo anapopeleka dawa hospitalini ni sisi tumesaidia, kwa hiyo kuongoza ni kusikiliza watu wanasema nini wakati mwingine.”

Mwananchi lilipotaka kujua hasa ni kitu gani ambacho anataka kumweleza Rais Magufuli, Rungwe amesema “hiyo ni siri yangu, lakini tumekuwa tikitafuta nafasi hiyo lakini wapi, lakini naona Lowassa kaenda na wamezungumza
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati. BOFYA HAPA KUJIUNGA NA INNOVATION FURSA CHALLENGE http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
UNGANA NASI KUPITIA LIKI HIZI ILI KUTUMIWA HABARI POPOTE ULIPO

EDUSPORTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI

WEKA EMAIL YAKO:


Delivered by EDUSPOTSTZ
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
EDUSPORTSTZ