BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Monday, 29 January 2018

BREAKINGNEWS; KITUO CHA JESHI NCHI AFGHANISTAN KIMEVAMIWA MUDA MCHACHE ULIOPITA
Milio ya risasi na milipuko imesikika katika kituo cha mafunzo ya kijeshi katika mji mkuu wa Afghanistan, Kabul, taarifa zinasema.

Vyombo vya habari vinasema Chuo Kikuu cha Masuala ya Ulinzi wa Taifa cha Marshal Fahim kimeshambuliwa mapema asubuhi.

Shambulio hilo limetokea baada ya shambulio lililowaua watu wengi zaidi miaka ya karibuni kusababisha vifo vya watu zaidi ya 100 Jumamosi.

Shambulio hilo la Jumamosi lilitekelezwa kwa kutumia gari la kubebea wagonjwa lililokuwa limejazwa vilipuzi.

Wapiganaji wa Islamic State na Taliban wamekuwa wakitekeleza mashambulio maeneo mbalimbali nchini humo.

Shambulio hilo la Jumamosi lilitekelezwa wiki moja baada ya shambulio jingine katika hoteli moja ya Kabul kuwaua watu 22 - wengi wao raia wa nchi za nje.

Taliban walisema ndio waliotekeleza mashambulio yote mawili.

Taasisi za kijeshi zimekuwa zikishambuliwa mara kwa mara na wanamgambo.

Oktoba 2017, makurutu 15 wa jeshi waliuawa kwenye mlipuko uliotokea nje ya kituo cha mafunzo ya kijeshi cha Marshal Fahim, ambacho hupatikana magharibi mwa Kabul. EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati. BOFYA HAPA KUJIUNGA NA INNOVATION FURSA CHALLENGE http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
UNGANA NASI KUPITIA LIKI HIZI ILI KUTUMIWA HABARI POPOTE ULIPO

EDUSPORTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI

WEKA EMAIL YAKO:


Delivered by EDUSPOTSTZ
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
EDUSPORTSTZ

No comments:

Post a Comment