UMOJA WA MATAIFA WAMPINGA TRUMP - EDUSPORTSTZ | Habari za Ajira, Mapenzi, Michezo, Elimu, Kilimo, Technology, Siasa na Mziki,

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Friday, 22 December 2017

UMOJA WA MATAIFA WAMPINGA TRUMP


Umoja wa mataifa kupinga maamuzi ya Trump

Mkutano mkuu wa Umoja wa mataifa umepiga Kura ya kutoyatambua maamuzi ya Marekani ya kuutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel.

Makubaliano hayo ya mkutano wa umoja wa mataifa yamefikiwa pamoja na vitisho vya Rais wa Marekani Donald Trump aliyetishia kuzikatia msaada wa kifedha nchi zote zitakazopinga msimamo wake.

Mataifa mia moja ishirini wameyapigiakura maazimio, baadhi ya mataifa hayo yakiwamo washirika wa karibu wa marekani yaani Japan, Uingereza na Ujerumani.

Canada na Mexico ni moja ya mataifa thelathini na tano ambayo hayakuhudhuria mkutano huo. Wapalestina wameiita hatua ya Umoja wa mataifa kuwa ni ushindi wa Palestina ingawa Israel imeyakataa matokeo.

Kabla ya kura, balozi wa marekani katika umoja wa mataifa, Bi Nikki Haley alionya kuwa Marekani haitasahau au kusamehe pale nchi zilizoipinga Marekani zitakapokuja kuomba misaada.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno

No comments:

Post a Comment