MANENO YA JPM BAADA YA KIFO CHA JOEL BENDERA - EDUSPORTSTZ | Habari za Ajira, Mapenzi, Michezo, Elimu, Kilimo, Technology, Siasa na Mziki,

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Thursday, 7 December 2017

MANENO YA JPM BAADA YA KIFO CHA JOEL BENDERA
Rais John Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa familia na wote walioguswa na kifo cha aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara Dr Joel Nkaya Bendera kilichotokea jioni ya leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa anapatiwa matibabu.

Rais ameeleza kuwa amesema marehemu atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa alioutoa kwa Taifa akiwa kiongozi katika nyadhifa mbalimbali zikiwemo Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Naibu Waziri na Mbunge na pia kwa mchango wake mkubwa katika maendeleo ya michezo.

“Dkt. Joel Nkaya Bendera alikuwa kiongozi shupavu, mahiri na mchapakazi, alipenda kufanya kazi kwa ushirikiano na daima alitamani kupata mafanikio makubwa katika majukumu aliyokuwa nayo, hakika tutamkumbuka” – Rais John MagufuliEDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno

No comments:

Post a Comment