-->

Type something and hit enter

On

Alikuwa miongoni mwa wanajeshi wanne wa Marekani ambao walihamia Korea Kaskazini miaka ya sitini na kuwa manyota wa filamu nchini humo

Mwanajeshi wa zamani wa Mareknai ambaye alihamia Korea Kaskazini na kuwa mfungwa kwa karibu miaka 40 amefariki.

Charles Jenkins, 77, aliishi nchini Japan ambapo alihamia na familia yake baada ya kuachiliwa mwaka 2004.

Alikuwa miongoni mwa wanajeshi wanne wa Marekani ambao walihamia Korea Kaskazini miaka ya sitini na kuwa manyota wa filamu nchini humo lakini ni yeye pekee aliweza kuachiliwa.

Wengine waliripotiwa kufariki wakiwa nchini Korea Kaskania akiwemo James Dresnok ambaye aliropitiwa kufariki kutokana na ugonjwa wa kiharusi mwaka 2016.
Bw Jenkins na familia yake waliondoka Korea Kaskazini mapema miaka ya 2000

Charles Jenkis alifariki akiwa kisiwa cha Sado siku ya Jumatatu ambapo alikuwa akiishi na mke wake Hitomi Sofa ambaye pia ni mfungwa wa zamani wa Korea Kaskazini.

Bw. Jenkins alikuwa akiishi maisha magumu akiwa nchini Korea Kaskazini ambayo alikuja kuyaelezea baadaye kwenye mahojiano kadhaa.

Mwaka 1965 akiwa na kikosi cha Marekani nchini Korea Kusini kilichokuwa eneo la mpaka wenye ulinzi mkali, Jenkins aliamua kukihama kikosi chake na kuhamia Korea Kaskazini akihofia kuwa angeua wakati wa doria au kutumwa kupigana vita huko Vietnam.

Alisema alifikiri kuwa akiwa nchini korea Kaskazini, akangeweza kuomba hifadhi kwenye ubalozi wa Marekani na baadaye kurudi Marekani wakati wa kubadilshwa kwa wafungwa.

CHANZO. BBC

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB

Click to comment