HIZI NDIZO SABABU ZA ZITTO KABWE KUKUTANA NA VIONGOZI WA VYAMA VYA UPIZANI - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

Friday, 22 December 2017

HIZI NDIZO SABABU ZA ZITTO KABWE KUKUTANA NA VIONGOZI WA VYAMA VYA UPIZANI

ACT-Wazalendo Yafunguka Sababu ya Zitto Kabwe Kukutana na Viongozi wa Upinzani

ACT-Wazalendo Yafunguka Sababu ya Zitto Kabwe Kukutana na Viongozi wa Upinzani

Baada ya kuenea kwa picha za Mwenyekiti wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe kuwa na baadhi ya viongozi wengine wa vyama vya upinzani hatimae chama hicho kimeeleza kuwa kiliazimia kuanza kufanya mazungumzo na viongozi wengine wa vyama vya upinzani ili kuunganisha nguvu kwenye mapambano ya demokrasia.

Akiongea na Bongo5 leo, Katibu Itikadi na Uenezi wa Chama hicho, Ndugu.Ado Shaibu amesema kuwa ingawa kila Chama kina Itikadi, sera na programu zake, yapo mambo ambayo Chama cha upinzani hakiwezi kufanya peke yake.

“Kamati Kuu ya Chama chetu iliazimia kuwa Uongozi wa juu wa Chama uanze mazungumzo na viongozi wengine wa Vyama vya upinzani ili kuunganisha nguvu kwenye mapambano ya demokrasia. Ingawa kila Chama kina Itikadi, sera na programu zake, yapo mambo ambayo Chama cha upinzani hakiwezi kufanya peke yake. Moja ya mambo hayo ni mapambano ya kidemokrasia kwa hiyo, Zitto amekwishafanya mazungumzo na Mbowe na Rungwe na atafanya mazungumzo na viongozi wa Vyama vingine,” amesema Ado.
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno