;
CHATU MKUBWA AWASHUTUA POLISI WAKIWA DORIA - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Thursday, 14 December 2017

CHATU MKUBWA AWASHUTUA POLISI WAKIWA DORIA


Polisi wa Queensland walipakia picha hiyo mtandaoni mara ya kwanza Jumatatu

Maafisa wawili wa polisi katika jimbo Queensland nchini Australia walipigwa na butwaa walipokumbana na chatu mkubwa wakipiga doria.


Ingawa walipigwa na butwaa mwanzoni, walitumia fursa hiyo kupiga picha na chatu huyo.

Picha ya mmoja wa polisi hao ilipakiwa mtandaoni na imezua hisia si haba.

"Nyoka huyo alikuwa na urefu wa zaidi ya mita tano, na kusema kweli si kiumbe ambaye unaweza kutafuta utepe useme utampima,"

Picha hiyo iliyopakiwa na polisi hao kwenye mitandao ya kijamii Ijumaa imetazamwa mara zaidi ya milioni mbili, na kutolewa maoni mara 10,000.

"Huwa hatufanyi mambo ya upweke," waliandika polisi hao.

"Huwa huwezi kujua utakutana na nini ukiwa kwenye zamu."


Polisi hao walikutana na nyoka huyo karibu na Wujul Wujul, karibu 345km (maili 210) kaskazini mwa jiji la Cairns.
Chatu aina ya Scrub, ambao huwa ndio nyoka warefu zaidi Australia, wanaweza kufikia urefu wa hadi 7m (futi 23).

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno

Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB