CCM YAMPATA MRITHI WA NYALANDU - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

DOWNLOAD AJIRA DAILY HAPA

Saturday, 16 December 2017

CCM YAMPATA MRITHI WA NYALANDU
Baada ya mchakato mrefu wa kura za maoni katika majimbo matatu yaliyokuwa yameachwa wazi likiwemo jimbo la Singida Kaskazini lililokuwa linashikiliwa Mhe. Lazaro Nyalandu, Hatimaye Chama cha Mapinduzi tayari kimetangaza majina matatu ya wagombea watakaosimama kuwania Ubunge kwenye majimbo hayo.
CCM imemsimamisha Monko Joseph kugombea jimbo la Singida Kaskazini ambalo liliachwa wazi na aliyekuwa mwanachama wao Lazaro Nyalandu.

Majina mengine ni Damas Ndumbaro jimbo la Songea Mjini, na Stephen Kiruswa jimbo la Longido.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu na Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa, Ndg Humphrey Polepole ameeleza kuwa wagombea hao kuanzia Kesho Desemba 16 wataanza kwenda kuchukua fomu NEC tayari kwa kujiandaa kwa uchaguzi mdogo.

Soma zaidi taarifa iliyotolewa na CCM;
JIUNGE NA BONGO5.COM SASA

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji


Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno