BADNEWS; ASKARI 14 WA TANZANIA WAUAWA - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

DOWNLOAD AJIRA DAILY HAPA

Saturday, 9 December 2017

BADNEWS; ASKARI 14 WA TANZANIA WAUAWA
Ijumaa ya December 8 2017 Tanzania imezipokea taarifa za wanajeshi 14 wa jeshi la wananchi Tanzania JWTZkuuwawa na waasi nchini DRC Congo, wanajeshi wa Tanzania walikuwa DRC Congo kama sehemu ya kikosi cha kulinda amani cha umoja wa mataifa UN.


Waasi wa ADF Jana Alhamisi ya December 7 2017 walivamia kambi ya MONUSCO iliyopo katika mji wa Beni na kufanya shambulio lililopelekea vifo vya askari 14 wa jeshi la wananchi wa Tanzania JWTZ na wamewajeruhi askari wengine 44 na wawili hawajulikani walipo.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Antonio Guterres amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kulaani vikali kitendo cha waasi wa msituni wa ADF kuwaua askari hao waliyokuwa DRC Congo kama sehemu ya kikosi cha kulinda amani cha UN.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno