ALIYEMUONDOA MUGABE MADARAKANI ATEULIWA KUWA MAKAMU WA RAIS - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

DOWNLOAD AJIRA DAILY HAPA

Thursday, 28 December 2017

ALIYEMUONDOA MUGABE MADARAKANI ATEULIWA KUWA MAKAMU WA RAIS


Jenerali wa zamani wa Jeshi Constantin Chiwenga ateuliwa kuwa makamu wa rais wa Zimbabwe

Aliyekuwa mkuu wa jeshi nchini Zimbabwe Constantin Chiwenga ameteuliwa kuwa makamu mpya wa rais wa Zimbabwe.

Bwana Chiwenga aliongoza jeshi kumtimua mamlakani aliyekuwa rais wa taifa hilo Robert Mugabe mnamo mwezi Novemba.

Alistaafu hivi majuzi na kuwa naibu wa chama tawala cha Zanu-Pf mnamo Disemba 23.

Naibu mwengine wa chama tawala cha Zanu-Pf ,aliyekuwa waziri wa maswala ya kigeni nchini Zimbabwe Kembo Mohadi pia atateuliwa kuwa makamu wa rais.
Jenerali Chiwenga aliyechukua mamlaka ya Mugabe
Jenerali wa jeshi aliyemng'oa Mugabe sasa ni naibu wa Zanu-PF
Rais Mugabe amtunuku shahada mke wa Jenerali aliyemzuia

Rais mpya Emmerson Mnangagwa alichukua mamlaka baada ya jeshi kuingilia kati mnamo tarehe 15 mwezi Novemba kufuatia mgogoro wa kumrithi Robert Mugabe.

Siku chache kabla ya jeshi kuchukua mamlaka , bwana Mnangagwa , wakati huo akiwa naibu wa rais alifutwa kazi na kuondoka nchini humo katika kile kilichoeleweka kuwa jaribio la rais kumpatia uongozi mkewe Grace kuwa mrithi wake.
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
UNGANA NASI KUPITIA LIKI HIZI ILI KUTUMIWA HABARI POPOTE ULIPO

EDUSPORTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI

WEKA EMAIL YAKO:


Delivered by EDUSPOTSTZ
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
EDUSPORTSTZ