WALIOITWA KWENYE USAILI UTAKAOFANYIKA KATI YA 2-7 DECEMBER - EDUSPORTSTZ

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Wednesday, 29 November 2017

WALIOITWA KWENYE USAILI UTAKAOFANYIKA KATI YA 2-7 DECEMBER

APPLICANTS WHO PASS INTERVIEW AND EMPLOYED AT PUBLIC SERVICE RECRUITMENT NOV 29
JAMHURI YA MUUNGANA WATANZANIA


OFISI YA RAIS


SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA


Kumb.NaEA.7/96/01/J/66 25 Novemba, 2017
TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI


Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Wizara,


Idara Zinazojitegemea, Taasisi za Umma MbalimbalI Serikalini, Sekretarieti za


Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa anapenda kuwataarifu waombaji kazi wote


walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 2-7


DESEMBA, 2017 na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi


watakaofaulu usaili huo.


Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo


yafuatayo:-

i. Usaili wa Mchujo utafanyika tarehe 2 DESEMBA, 2017 kama ilivyoainishwa


kwenye tangazo hili, muda na sehemu usaili ambapo usaili utafanyika


umeainishwa kwa kila Kada;

ii. Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;

iii. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi,


Kitambulisho cha Mpigakura, Kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Uraia


au Hati ya kusafiria;

Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha


kuzaliwa, kidato cha IV, VI, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na


kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji;


v. Wasailiwa watakaowasilisha“Testimonials”, “Provisional Results”, “Statement


of results”, hati za matokeo za kidato cha IV na VI (form iv and form vi


results slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA


NA USAILI;

vi. Kila msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi;

vii. Kila Msailiwa azingatie tarehe na mahali alipopangiwa kufanyia usaili;

viii. Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao


vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika (TCU na NECTA); na

ix. Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili


watambue kuwa hawakukidhi vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi


nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji yaTangazo husika.

x. Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma


wanapaswa kuja na vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za


kufanyia kazi.

kusoma ratiba ya usalili na majina bofya hapo chini

Download attachments:
KUITWA_KWENYE_USAILI_1.pdf
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno

No comments:

Post a Comment