TAMBWE AJITABIRIA MAKUBWA LICHA YA KUSUMBULIWA NA MAJERAHA - EDUSPORTSTZ | Habari za Ajira, Mapenzi, Michezo, Elimu, Kilimo, Technology, Siasa na Mziki,

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Saturday, 18 November 2017

TAMBWE AJITABIRIA MAKUBWA LICHA YA KUSUMBULIWA NA MAJERAHADar es Salaam. Mshambuliaji wa Yanga, Amiss Tambwe amaenza mazoezi rasmi na wenzake
 iliyopita, huku akiahidi kuwashangaza watu kwa kuondoka na kiatu cha dhahabu.

 Tambwe ambaye aliumia goti la kushoto mazoezini siku chache kabla ya mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Simba hajacheza mechi tisa na kesho Jumapili Yanga itacheza mechi ya 10 bila Tambwe ambaye anasema kama mambo yasipobadilika ataanza kuonekana uwanjani kabla hata ya Krismasi. 

 "Nafarijika kuona kidogo nimeanza kuwa fiti japo nimekatazwa kufanya mazoezi ya nguvu hadi niimarike zaidi vinginevyo mambo yatakuwa ndivyo sivyo," alisema mshambuliaji huyo. 

Tambwe ambaye aliwahi kusema kwamba hajui anaumwa nini kutokana na vipimo kutoonyesha ugonjwa kwenye goti lake zaidi ya mara nne amesema haofii mechi zilizokwishachezwa kwenye Ligi Kuu hadi sasa, lakini mpango wake ni kuchukua kiatu cha dhahabu mwishoni mwa msimu.

  "Ligi bado sana, najua nitakosa mechi kama 12 hadi 14 za mzunguko wa kwanza, lakini  nitakapokuwa fiti na kuanza kucheza lazima nitimize ndoto yangu ya kuwa mfungaji bora," alisema. Akizungumzia mazoezi yake ya kwanza na wenzake, Tambwe alisema yalikuwa ya kukimbia na kubainisha kwamba yamemsaidia kuimarisha afya yake kwani hivi sasa maumivu kwenye goti lake yameanza kupungua. 

Kiukweli nilikuwa sijui naumwa nini, maana nilipimwa zaidi ya mara nne, madaktari hawakuona chochote, nikaamua kusali na kufanya mazoezi binafsi ya tumbo na kukimbia ufukweni hadi nilipojiunga na wenzangu wiki hii. 

"Bahati nzuri ni kwamba baada ya mazoezi na wenzangu maumivu yameanzakupungua ingawa nimeshahuri nisifanye mazoezi magumu hadi nitakapokuwa fiti zaidi," alisema. Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno

No comments:

Post a Comment