POLISI WAFANYA UPEKUZI MAKAO MAKUU YA ACT WAZALENDO - EDUSPORTSTZ

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Wednesday, 8 November 2017

POLISI WAFANYA UPEKUZI MAKAO MAKUU YA ACT WAZALENDO


Polisi Wafanya Upekuzi Makao Makuu ya ACT Wazalendo, Waondoka na Nyaraka, Vifaa vya Kielektoniki

Jeshi la Polisi limefanya upekuzi Makao Makuu ya Chama cha ACT- Wazalendo na kuchukua nyaraka, vifaa vya kiilektonikia vilivyotumika kuandaa taarifa ya kusinyaa kwa uchumi wa nchi.

Upekuzi huo umefanyika leo mchana muda mfupi baada ya Zitto kwenda kuripoti Kitengo cha Uhalifu wa Makosa ya Kifedha Kamata jijini Dar es salaam na kutakiwa kurejea tena Novemba 21.
Taarifa iliyotolewa jioni hii na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Ado Shaibu amesema polisi walifika ofisini hapo saa 6 mchana na wameondoka mida ya saa 10 na wamechukua flash, laptop (kompyuta mpakato) na nyaraka ambazo ni taarifa kwa umma iliyotolewa kupitia wanahabari.
Ado amesema kwamba “Wamesema watakwenda kufanyia kazi vifaa hivyo na watavirejesha haraka ila hawajasema hasa ni lini," ameongeza
Mapema leo Jeshi hilo la polisi lilishikilia simu ya mkononi ya Kiongozi wa chama hicho, Zitto Kabwe kwa upelelezi huku yeye akisema mawasiliano aliyokuwa akiyafanya yamezingatia uhuru ulipo katika Katiba.
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno Propellerads

For Booking>>>CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI
No comments:

Post a Comment