MBOWE HANA HOFU YA TUHUMA ZA UFISADI DHIDI YA NYALANDU - EDUSPORTSTZ

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Thursday, 16 November 2017

MBOWE HANA HOFU YA TUHUMA ZA UFISADI DHIDI YA NYALANDU


MBOWE: “Wachunguzeni Lowassa, Sumaye na Nyalandu” Hatuogopi

Ni maneno ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Freeman Mbowe akiwa Mbeya kuendelea na ziara ya kuwanadi Wagombea wa Udiwani katika uchaguzi mdogo.

Mbowe akiwa jukwaani amesema “Nimemsikia Waziri mmoja, Waziri Kigwangalla……. anatoa maelekezo kwa TAKUKURU wamshughulikie Lazaro Nyalandu aliekua Waziri wao ambae sasa hivi fresh ndani ya CHADEMA“


“Wakasema CHADEMA mlisema Lowassa alikua fisadi tukawaambia sawa tulisema kwa wakati wake, kwenye siasa hauna Rafiki wa kudumu wala Adui wa kudumu lakini tumeshtuka kwamba huo ufisadi wake hamjaweza kuudhihirisha, mpelekeni Mahakamani…….. hawana cha kupeleka Mahakamani”

“TAKUKURU wanasema wameshapewa malalamiko kwahiyo wanayafanyia kazi tunawaambia CHADEMA hatuogopi Mahakama na kiongozi yeyote ndani ya CHADEMA mnaetaka kumchunguza akiwemo Mbowe anzeni leo hatuogopi”

“Awe ni Lowassa mchunguzeni, awe ni Sumaye mchunguzeni… awe ni Nyalandu mchunguzeni, awe ni Sugu mchunguzeni”

Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno

No comments:

Post a Comment