ASKOFU ATUMIA POMBE KATIKA UBATIZO - EDUSPORTSTZ | Habari za Ajira, Mapenzi, Michezo, Elimu, Kilimo, Technology, Siasa na Mziki,

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Saturday, 4 November 2017

ASKOFU ATUMIA POMBE KATIKA UBATIZO



Mchungaji mmoja huko Afrika Kusini amekuwa akikosolewa vikali baada ya kuanza kubatiza washirika kwa kutumia vilevi ambavyo wanavipenda kitendo ambacho ni kinyume na utaratibu.
Askofu Tsietsi Makiti, (52) ambaye pia ni Mwanzilishi wa kanisa hilo linalojulikana kama 'Gabola', amesema kuwa ameongozwa na maandiko katika Biblia ambapo Yesu alibadilisha maji kuwa divai.

"Watu wanao kunywa na kubatizwa na bia wana furaha na amani. Hii inamaanisha kuwa wanaishi katika kivuli cha Mungu, "alisema Makiti.

Kanisa hilo lenye jina 'Gabola' jina likimaanisha 'Kunywa' limesema linakubali kuwapokea waumini waliotoka makanisa mengine huku likiweka wazi kwamba idadi ya watu wameongezeka kufikia 500 ndani ya miezi miwili tangu kuanzishwa kwa kanisa hilo.

Waumini pia wanaruhusiwa kunywa wakati huduma za kanisa zikiendelea.

Aidha Askofu huyo ameweka wazi kwamba ana mipango ya kuanzisha matawi ya kanisa lake hilo katika miji mbali mbali.
like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika 
Edusportstz
TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA
For Booking>>>
EMAIL: edusportstz@gmail.com
CALL>>>
Voda: +255757441463
JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI
INSTAGRAM
FACEBOOK
SUBSCRIBE YOUTUBE CHANEL
DOWNLOAD EDUSPORTS ANDROID APPLICATION CLICK HERE

Follow @bakalemwatz

No comments:

Post a Comment