MAHAKAMA YA JUU YASITISHA UCHAGUZI WA RAIS - EDUSPORTSTZ

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Wednesday, 1 November 2017

MAHAKAMA YA JUU YASITISHA UCHAGUZI WA RAIS


Mahakama ya juu yasitisha uchaguzi wa rais Liberia


George Weah (kushoto) na makamu wa Rais Joseph Boakai

Mahakama ya juu zaidi nchini Liberia imeamrisha maandalizi ya duru ya pili ya uchaguzi wa urais kusitishwa kufuatia madai ya udanganyifu kutoka kwa mgombea aliyeondolewa kutoka kinyanganyiro hicho.

Mcheza soka wa zamani George Weah na makamu wa Rais Joseph Boakai wanatarajiwa kukutana katika duru hiyo ya pili ya tarehe 7 Novemba.

Lakini mgombea wa chama cha Liberty Charles Brumskine, ambaye alichukua nafasi ya tatu amepinga matokeo hayo.

Uchaguzi wa mwezi uliopita ndio wa kwanza huru kufanyika tangu viishe vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2003.

Mahakama imeamrisha chama cha Liberty na tume ya uchaguzi nchini humo kupeleka kesi zao ifikapo Alhamisi.

Lakini msemaji wa tume ya uchaguzi Henry Flomo aliambia BBC kuwa hajajulishwa rasmi kuhusu amri hiyo ya mahakama.

Waangalizi wa kimataifa wakimemo wale kutoka muunganoa wa Ulaya hajaezea hitilafu yoyote wakati wa duru ya kwanza ya uchaguzi.


 like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI
No comments:

Post a Comment