KUHAMA KWA NYALANDU KWAGUBIKWA UTATA MTUPU - EDUSPORTSTZ | Habari za Ajira, Mapenzi, Michezo, Elimu, Kilimo, Technology, Siasa na Mziki,

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Wednesday, 1 November 2017

KUHAMA KWA NYALANDU KWAGUBIKWA UTATA MTUPU


Hii Hapa Barua ya Katibu Mkuu CCM Kuhusu Kujiuzulu kwa Nyalandu

Baadae Spika Ndugai alihojiwa na vyombo vya habari na kusema kwamba pamoja na kusikia taarifa za kujiuzulu kwa Nyalandu kwenye vyombo vya habari, yeye bado hajapokea barua ya kujiuzulu kwa Mbunge huyo.

Sasa leo imetoka taarifa kutoka Ofisi ya Bunge Dodoma ikiwa imeandikwa kama inavyosomeka hapa chini…

Ofisi ya Spika ingependa kuwaarifu Watanzania wote kwamba mpaka sasa haijapokea barua toka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini (CCM) Ndugu Lazaro Nyalandu ambayo amekuwa akiarifu kwamba amemwandikia Mheshimiwa Spika kumtaarifu kujiuzulu kwake.

Hata hivyo, Mhedhimiwa Spika amepokea barua toka kwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi ya tarehe 30 Oktoba, 2017 akimuarifu kwamba kwa muda sasa Chama hicho kilishaanza kumchukulia hatua za kiudhibiti na kinidhamu dhidi ya vitendo na kauli zake zisizoridhisha kinyume na misingi, falsafa na itikadi ya Chama cha Mapinduzi.

Hivyo, Chama cha Mapinduzi kuanzia tarehe ya barua yao kimemjulisha Mheeshimiwa Spika kuwa Ndugu Lazaro Nyalandu amepoteza sifa za Uanachama wa Chama cha Mapinduzi, na hivyo kupoteza nafasi zote za uongozi wa ndani wa Chama hicho na Ubunge kwa mujibu wa Ibara ya 13 ya Chama hicho.

Mheshimiwa Spika, angependa kuwaarifu Watanzania kwamba kwa barua hiyo toka mamlaka halali ndani ya Chama cha Mapinduzi ambacho Ndugu Lazaro Nyalandu alipata Ubunge kupitia Chama hicho na kwa mujibu wa Ibara ya 71 (1)(f) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayotamka kwamba:

“Mbunge atakoma kuwa Mbunge na ataacha kiti chake cha Ubunge iwapo litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo: (f) Iwapo Mbunge ataacha kuwa Mwanachama cha chama alichokuwamo wakati alipochaguliwa au alipoteuliwa kuwa Mbunge.”

Hivyo, Ndugu Lazaro Nyalandu si Mbunge tena na hatua stahiki za kuiarifu Tume ya Taifa ya Uchaguzi zinaendelea kuchukuliwa.

Imetolewa na: Ofisi ya Spika S.L.P. 941

DODOMA

Ofisiya Bunge S.L.P 941 DODOMA

01 Novemba 2017like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI
No comments:

Post a Comment