JOSHUA NASSARI AKATA RUFAA KUENGULIWA KWA WAGOMBEA UDIWANI - EDUSPORTSTZ | Habari za Ajira, Mapenzi, Michezo, Elimu, Kilimo, Technology, Siasa na Mziki,

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Wednesday, 1 November 2017

JOSHUA NASSARI AKATA RUFAA KUENGULIWA KWA WAGOMBEA UDIWANI


Hii Hapa Sababu ya Joshua Nassari, Kukata Rufaa

Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassari, amekata rufaa kupinga hatua ya kuenguliwa wagombea wake wawili waliopitishwa kugombea udiwani kwenye uchaguzi mdogo wa marudio unaofanyika katika kata tano katika Jimbo la Arumeru Mashariki.

Akizungumza na waandishi wa habari, Nassari amesema kuwa amesikitishwa na uamuzi uliofanywa na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi huo kwani hawakuzingatia kanuni, taratibu na sheria za uchaguzi.
Nasari amesema amekata rufaa Tume ya Uchaguzi kupitia Mkurugenzi wa Taifa wa Uchaguzi kufikisha malalamiko yao kwani kutenguliwa kwa wagombea wao kutokana na kutofuatwa taratibu ikiwemo Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi kuwatengua wagombea wakati hana sifa ya kufanya hivyo
"Mapingamizi yaliyowekwa hayakuwa na mashiko Wagombea wetu wameenguliwa kinyume cha sheria. Na suala hili la kuenguliwa limekuja baada ya majaribio ya utekaji, fedha kutumia washawishi wakiwa viongozi wa mila, vitisho vya uhai wao kushindikana," Nassari.
Hata hivyo Nassari amesema alilazimika kuwahifadhi wagombea hao nyumbani kwake ili kuwaepusha na madhila pamoja na mitego waliyokuwa wamewekewa.like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI
No comments:

Post a Comment