IJUE KIUNDANI VITA YA KOREA KASKAZINI VS MAREKANI - EDUSPORTSTZ

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Monday, 6 November 2017

IJUE KIUNDANI VITA YA KOREA KASKAZINI VS MAREKANIWiki iliyopita tuliona sarakasi za Kim Jong-un, kiongozi wa Korea Kaskazini ambaye ni mtu korofi dhidi ya taifa lenye nguvu duniani la Marekani, lakini mwenye maajabu yake juu ya kupenda vita. SASA ENDELEA…
UKWELI ni kwamba Kim Jong-un anaaminika kuwa ni mtu hatari kwa dunia ya sasa kwani alimhukumu kifo kamanda msaidizi wa jeshi la wananchi wa Korea Kaskazini kwa kosa la kuhudhuria msiba wa baba yake akiwa amelewa.

Alitoa amri kwamba ‘anyongwe na usibaki hata unywele wake’, jambo ambalo lilitekelezwa. Kama hiyo haitoshi, Kim Jong-un pia alitoa hukumu ya kifo kwa mjomba wake kwa kile kilichodaiwa kuwa alitenda kosa la ubadhilifu wa mali ya umma na harakati za kupindua nchi hiyo.

Huyu aliamuru avuliwe nguo na kutupwa katika banda la mbwa wakali waliomzika kwenye matumbo yao. Mmoja kati ya marafiki wakubwa wa Kim Jong-un ni nyota wa zamani wa NBA, Dennis Roadman. Akiwa mwanafunzi, Kim Jong-un alitumia muda wake mwingi kuchora picha za Dennis Roadman.

Huyo ndiye Kim Jongun, rais anayewanyima amani Korea Kusini na mshirika wake mkubwa, Marekani. Anadai yupo tayari kwa lolote dhidi ya Marekani hasa kwa nguvu za kinyuklia. Anaendeleza kile walichokiamini babu na baba yake kuwa Marekani ndiyo adui mkubwa wa Korea Kaskazini. Kim Jong-Un amekuwa akisisitiza kuwa yupo tayari kwa vita dhidi ya Marekani hata kama akiwa yupo usingizini.

Hayo aliyasema katika sherehe za mwaka huu katika Maadhimisho ya Miaka 70 tangu kubuniwa kwa chama tawala nchini humo. Kiongozi huyo amekuwa akitoa maelekezo kwa maelfu ya wanajeshi ya namna ya kutumia vifaru na magari yanayoweza kuzuia mabomu na makombora. Kwenye hotuba yake ya kwanza kwa umma kwa miaka mitatu, Kim alionekana mwenye hasira zaidi ikilinganishwa na hotuba zake za awali ambapo alitoa ujumbe maalum kwa adui yeyote wa nchi hiyo.

Huku akishangiliwa na maelfu ya wananchi, Kim anasema: “Chama chetu kinatangaza kuwa majeshi yetu yana uwezo wa kupigana aina yoyote ya vita itakayoanzishwa na Marekani.” Juu ya uwanja kulikuwa na bango lililoelea hewani lenye maandishi yaliyosomeka; “Chama imara cha Worker’s Party of Korea (WPK) kidumu maisha marefu zaidi.”

Tishio la Korea Kaskazini kuiangamiza Marekani na nchi jirani ya Korea Kusini si jipya, ingawa wakati huu lilitolewa kwa njia ya ukaidi zaidi kwani ilikuwa katika hafla ya umma, mbele ya kamera za vituo vya habari vya kimataifa. Baada ya hotuba yake ya dakika 20, wanajeshi walianza maonesho yao ambapo waliandamana na picha kubwa za babu yake na baba yake wakitabasamu kuashiria ushindi.

Dhamira kuu ya hafla hiyo ilikuwa kukisifu chama tawala cha Worker’s Party ambacho kimekuwa madarakani kwa vizazi vitatu vya familia ya Kim kwa miongo saba sasa. Maonesho ya vifaa vya kijeshi vya nchi hiyo ndiyo huvutia zaidi mataifa ya kigeni ambayo hujaribu kuchunguza kama kuna teknolojia yoyote mpya inayotumiwa na nchi hiyo katika utengenezaji wa vifaa vya kivita.

Pia wana makombora makubwa yanayoweza kurushwa hatua za mbali ambazo zimewahi kuoneshwa katika mwaka wa 2012 na 2013 ambazo kila wakati huvutia mjadala kuhusu ikiwa ni silaha zinazoweza kutumika au la kama inavyoaminika. Je, nini kiliendelea? Usikose wiki ijayo.

 like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika
Propellerads

For Booking>>>CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI
No comments:

Post a Comment