HOFU NA HATARI KUTANDA KULIPUKA KWA MLIMA WA VOLCANO BALI - EDUSPORTSTZ | Habari za Ajira, Mapenzi, Michezo, Elimu, Kilimo, Technology, Siasa na Mziki,

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Monday, 27 November 2017

HOFU NA HATARI KUTANDA KULIPUKA KWA MLIMA WA VOLCANO BALIMaafisa wanasema mlma huo wa volkano umekuwa ukitoa moshi mkubwa mfululizo

Mamlaka nchini Indonesia imetangaza hali ya tahadhari kubwa kufuatia kuwepo dalili za kutokea mlipuko mkubwa wa Volcano katika mlima wa Agung.

Uwanja wa ndege wa kipekee katika kisiwa hicho maarufu cha utalii cha Bali umefungwa.

Majivu na moshi wa Volcano hiyo imefikia urefu wa zaidi ya mita 3000 juu ya mlima huo hali iliyosababisha giza.

Mlima huo uitwao Agung ulirusha majivu mengi na kutandaza mvuke na moshi mwingi mara ya pili katika kipindi cha wiki moja.

Maafisa wamehimiza na kuwasaidia maelfu ya wakaazi na watalii kulihama ene hilo na kwenda kwingine.

Mwaka 1963 mlima huo ulilipuka na kusababisha vifo vya takriban watu 1,600.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno

No comments:

Post a Comment