FIGISU ZA PLUIJM ZILIMFICHA KWAPANI TSHISHIMBI - EDUSPORTSTZ | Habari za Ajira, Mapenzi, Michezo, Elimu, Kilimo, Technology, Siasa na Mziki,

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Monday, 6 November 2017

FIGISU ZA PLUIJM ZILIMFICHA KWAPANI TSHISHIMBI

 tshishimbi
KOCHA Mkuu wa Singida United, Mholanzi, Hans van Der Pluijm, juzi Jumamosi alimkomoa kiungo wa Yanga, Papy Kabamba Tshishimbi baada ya kumpangia viungo watatu wamkabe kwenye mechi iliyozikutanisha timu hizo mbili.
Juzi Jumamosi, Singida United ikiwa kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Namfua, ilitoka suluhu na Yanga katika mwendelezo wa Ligi Kuu Bara, huku Tshishimbi raia wa DR Congo aliyetarajiwa kuwika, akibanwa vilivyo.

Katika mchezo huo, Pluijm aliwapanga Mzimbabwe, Tafadzwa Kutinyu, Mudathir Yahya na Kenny Ally, ili wamdhibiti Tshishimbi ambapo hali hiyo ilimfanya kiungo huyo wa Yanga kuwa na wakati mgumu kila alipopanga mikakati ya mashambulizi.

Kutokana na kubanwa huko, Tshishimbi alimaliza dakika tisini akipiga shuti moja pekee lililotoka nje ya lango na ambalo halikuwa na nguvu. Pluijm alifanya hivyo baada ya kuutambua uwezo wa Tshishimbi ambao ameuonyesha kwenye mechi kadhaa zilizopita za ligi kuu ikiwemo dhidi ya Simba.

Stori: Sweetbert Lukongelike facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI
No comments:

Post a Comment