WAFAHAM MARAIS KUMI WA AFRIKA WALIOFARIKI WAKIWA MADARAKANI - EDUSPORTSTZ | Habari za Ajira, Mapenzi, Michezo, Elimu, Kilimo, Technology, Siasa na Mziki,

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Wednesday, 18 October 2017

WAFAHAM MARAIS KUMI WA AFRIKA WALIOFARIKI WAKIWA MADARAKANIAfrika ni bara lenye historia kubwa toka enzi hizo za Mababu, ni bara ambalo lina rekodi zake nyingi tu ikiwemo Marais waliokaa madarakani muda mrefu bila kuachia kiti, lakini pia kumbukumbu ya leo inawakumbuka Marais 10 ambao waliuwawa wakiwa madarakani.
Muhammad Anwar El-Sadat

Huyu alikuwa rais wa Misri ambae aliuawa akiwa na umri wa miaka 62, kabla ya kuwa Rais wa misri El Sadat alikuwa Makamu wa rais wa nchi hiyo kipindi ambacho Rais alikuwa Gamel Abdel Nasser.

Kabla ya kuuawa Elsadat alikuwa kiongozi maarufu na aliependwa sana na watu wake kwa kazi mbalimbali alizozifanya ikiwa ni pamoja na kuleta amani kati ya Misri na taifa la Israel hadi kufikia kusaini makubaliano ya amani baina ya nchi hizo mbili na hiyo ikafanya apewe Tuzo ya heshima ya Amani yaani Nobel Peace Prize

Hata hivyo suala hili halikuwafurahisha watu wote hususani baadhi wa wafuasi wa dini ya kiislamu ambao walipanga mashambulizi juu yake na hatimaye Oktoba 6 mwaka 1981 Ofisa wa jeshi aliyejulikana kama Islambaili alimuua kwa kumpiga risasi kadhaa Rais elsadaat.

Islam Baili alikamatwa baada ya amuda mfupi wa kuhukumiwa kifo kutokana na tukio hilo.Juvenal Habyarimana

Huyu alikua kiongozi wa nchi ya Rwanda alieuawa akiwa na miaka 57 baada ya kuongoza nchi yake kwa miaka 21 ambapo aliingia madarakani kwa kupindua nchi akiwa na miaka 36 na ikafanya idadi ya maadui zake iongezeke.

April 6, 1994 akiwa kwenye ndege ambayo ilikua inajiandaa kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kigali, Rais Habyarimana akiwa na rafiki yake ambae pia alikua ni Rais wa Burundi Cyprien Ntaryamira ndege yao ililipuliwa na miili yao haikutambulika kabisa.

Mauaji haya ya viongozi hawa wa juu wa Serikali za nchi zao yalichangia kwa kiasi kikubwa kuanza kwa Mauaji ya kimbari Rwanda ambayo yalisababisha vifo vingi.Laurent Kabila

Rais mwingine aliyeuawa ni Laurent Kabila ambaye alikua na miaka 61 wakati anauawa, alikuwa ni wa nchi ya Zaire ambayo baadae ilikuja kuitwa Jamhuri ya Demokrasia ya Congo DRC…. Laurent aliingia madarakani baada ya kuupindua utawala wa Mobutu SeseSeko ambaye nae aliingia madarakani kwa kuipindua Serikali iliyopita.

Kabila alikua ni mfanyabiashara lakini aliamua kuacha kazi hiyo na kuamua kuingia kwenye vita ya kwanza ya Congo DRC na baada tu ya kumuondoa Mobutu alianza kufanya mageuzi ndani ya Serikali.

Mchana wa tarehe 18 january 2001, mmoja ya Walinzi wake alimpiga risasi kadhaa na kutaka kukimbia lakini hakufanikiwa kwani aliuwawa na Maaskari wengine papohapo…. Laurent kabila alitibiwa kwa siku mbili kabla ya kufariki

Siku 10 baada ya kifo chake mwanae ambae ni Joseph Kabila alichukua nafasi ya baba yake na kuwa rais wa DRC mpaka leo.Melchior Ndadaye

Huyu alikuwa rais wa Bururndi na aliuawa akiwa na miaka 40 October 21, 1993, Melchior alikuwa Raisi wa kwanza kutoka kabila la Wahutu kuchaguliwa kidemokrasia nchini Burundi mwaka 1993.

Watu wa kabila wa Watutsi hawakufurahishwa na ushindi huo na wiki moja kabla ya kuapishwa kuingia madarakani jaribio la kumuua lilifanyika lakini halikufanikiwa, hata hivyo karibu miezi mitatu tu toka akalie kiti cha Urais akauwawa na Jeshi la waasi wa kabila la Watutsi.Cyprien Ntaryamira

Huyu ni rais ambaye aliingia madarakani kuziba pengo la Rais wa Burundi Melchior Ndadaye alieuwawa October 1993, miezi sita tu baada ya kuingia madarakani Cyprien Nyaryamira nae aliuawa.

Huyu ndie alikua pamoja kwenye Ndege na Rais wa Rwanda Juvenal Habyarimana baada ya ndege yao kulipuliwa angani ilipokuwa inajiandaa kutua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kigali.Mohamed Boudiaf

Rais Mohamed Boudiaf alikuwa ni Raisi wa Algeria na aliuawa akiwa ma miaka 73 mwaka 1992 huku ikielezwa kuwa alikua kiongozi mkali na hakuvumilia uzembe na hiyo ikamfanya apate maadui wengi.

Majaribio mbalimbali ya kumuua yalifanyika dhidi yake na hata kuna kipindi aliamua kutoroka kwenye nchi yake ili aende kujificha na kukimbia wanaomuwinda lakini baada ya kujificha kwa miaka 27 akiwa Morocco katika hali ya kushangaza aliombwa kuongoza mapinduzi ya nchi yake ya Algeria na baadae kuchukua uongozi wa nchi hiyo kama rais.

Miezi minne tu baada ya kuingia madarakani June 29, 1992 Boudiaf aliuawa na Mlinzi wake wakati akiwa anatoa hotuba kwenye kipindi cha Televisheni ikiwa ni mara ya kwanza kwenda nje ya Algiers kama rais.Bare Mainassara

Bare alikua kiongozi wa Serikali ya Niger na aliuawa akiwa na umri wa miaka 49 April 9, 1999, alichukua uongozi kwa kufanya mapinduzi ya serikali na kwa kuwa kitendo hicho kilisababisha watu wengi wamchukie aliamua kuanza mchakato wa kufanya suala hilo la mapinduzi kuwa la kisheria.

Aliamua kuandaa uchaguzi wa kidemokrasia ambao alishinda kwa asilimia 52, upinzani walichukizwa na ushindi huo kwani waliamini si wa kweli na kushinikiza matokeo hayo yafutwe lakini Bare hakukubali kuachilia kiti hicho.

Jeshi liliamua kuingilia kati suala hilo na Rais Bare aliuawa kwa kupigwa risasi alipokua akielekea kupanda helikopta katika uwanja wa ndege wa Niamey na kiongozi wa mapinduzi hayo Daouda Malam Wanke akachukua kiti chake.Samuel Doe

Aliongoza nchi ya Liberia kabla ya kuuwawa mwaka 1990 akiwa na miaka 39 ambapo kabla ya Samuel Doe kuingia madarakani nchi hiyo ilikuwa chini ya utawala wa Wamarekani wenye asili ya Liberia kwa zaidi ya karne mpaka kiongozi huyu alipoongoza mapinduzi ya kijeshi yaliyomuuwa Rais William Tolbert Jr.

Mawaziri wa Rais alieuawawa pia waliuawa hadharani siku 10 tu baada ya tukio hilo la boss wao na Doe akawa kiongozi wa kwanza mwenye asili halisi ya Liberia na kuongoza kwa miaka 10.

Mwaka 1989 Desemba ilitokea vita ya wenyewe kwa wenyewe baada ya rafiki wa zamani wa Samuel Doe, Charles tayllor aliyekuwa amefungwa katika gereza moja Marekani kutoroka na kuunda kikundi cha waasi na kuingia Liberia kupitia Cote d’Ivoire kwa nia ya kufanya uasi.

Siku chache baadae Rais Doe alikamatwa na kikundi hicho na kuteswa sana kisha kuuawa September 9, 1990 na baadae mwili wake ulipitishwa kwenye mitaa ya Monrovia ukiwa mtupu ili watu wauone.Thomas Sankara

Yeye alikuwa Rais wa nchi ya Upper Volta alieongoza nchi yake kwa miaka minne tu kabla ya kuuwawa akiwa na miaka 37, Sankara alipata uongozi kwa njia ya mapinduzi ya kijeshi pia akiwa na miaka 33.

Inaelezwa kuwa Sankara alichochea maendeleo ya uchumi kwa kiasi kikubwa sana nchini humo na hata kubadilisha jina la nchi yake Upper Volta kuwa Burkina Faso ikiwa na maana ya nchi ambayo watu wake sio wala rushwa.

Alikuwa pia raisi wa kwanza Afrika kuteua Wanawake kushika nafasi za juu kwenye baraza lake la mawaziri, baada ya miaka minne tangu aingie madarakani Sankara aliuawa 15 October 1987 baada ya serikali yake kupinduliwa na rafiki yake wa zamani Blaise Compaore.

Sankara anatajwa kuwa kiongozi aliyependwa sana na watu na hata vitabu vingi vimendikwa kwa kumbukumbu na heshima yake.Muammar Gaddafi

Huyu alikuwa Rais wa Libya ambaye ndiye Rais alieongoza nchi hiyo kwa kipindi kirefu zaidi na kama angekuwa hai hadi sasa ndiye ambaye angeshikilia rekodi ya kiongozi wa Afrika aliyekaa madarakani kwa kipindi kirefu akifuatiwa na Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe.

Gaddafi aliingia madarakani baada ya kuupindua uongozi wa Mfalme Idris na kufanya nchi hiyo kuongozwa chini ya Serikali ya Jamhuri na kukaa madarakani kwa miaka 42 kabla ya kuuwawa.

Inaripotiwa mwaka 2011 yalitokea mapigano nchini humo ya baadhi ya watu kumpinga Muammar Gaddafi ambayo yalipelekea vita vya wenyewe kwa wenyewe na ndipo Marekani na Nato walipo waunga mkono Waasi na kumuangusha serikali ya Gaddafi.

October 20, 2011 Gaddafi akiwa na miaka 69 alikamatwa na kuuawa na huo ukawa mwisho wa uongozi uliokaa kwa miaka mingi kuliko yote duniani.


like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI
No comments:

Post a Comment