UDART YATOA YA MOYONI JUU YA OFISI ZAO KUKUBWA NA MAFURIKO - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

Sunday, 29 October 2017

UDART YATOA YA MOYONI JUU YA OFISI ZAO KUKUBWA NA MAFURIKO


Image result for udart tanzania

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha Udart, Deus Bugaywa, alipozungumza na wanahabari.

KAMPUNI ya usafiri wa mabasi ya mwendo kasi jijini Dar es Salaam (Udart) imeeleza athari ilizozipata kutokana na mafuriko yaliyotokea Alhamisi wiki hii katika eneo la Jangwani ambako magari ya mwendokasi huegeshwa na imewaomba wateja wake radhi pale kutokana na adha ya usafiri kwa siku hiyo.

Akizungumza na wanahabari jana, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha Udart, Deus Bugaywa, alisema mabasi 29 kati ya 134 yanayotoa huduma yaliathirika kutokana na kuingiliwa maji sehemu mbalimbali za magari hayo zikiwemo injini.

“Tunaomba radhi kwa wateja wetu kutokana na usumbufu walioupata mafuriko yalipotokea siku ya Alhamisi katika jiji la Dar es Salaam na kusababisha huduma zetu kutokufanya kazi zake ipasavyo. Hivyo, mabasi yetu 29 yalishindwa kuendelea kutoa huduma lakini juhudi za haraka zinaendelea kufanyika kwani mafundi wetu wanafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha usafiri unarejea kama zamani,” alisema.

Aliongeza kwamba wamelazimika kuhamisha baadhi ya shughuli na kuziondoa katika eneo la Jangwani, hivyo baadhi ya magari kulazimika kuegeshwa kituo cha Gerezani na Kivukuoni.

NA DENIS MTIMA/GPL

 like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI