SHUHUDIA PICHA ZA LISSU MARA BAADA YAKUTOKA NJE KWAMARA YA KWANZA - EDUSPORTSTZ

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Thursday, 19 October 2017

SHUHUDIA PICHA ZA LISSU MARA BAADA YAKUTOKA NJE KWAMARA YA KWANZAFamilia ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu imesema kwamba kwa mara ya kwanza ndugu yao alipotolewa nje kupata hewa na kuota jua kauli yake aliyoitoa alisema kuwa ni sawa na ukiwa mfungwa huoni jua, mawingu wala hupigwi upepo wa kawaida.


Katika mahojiano aliyofanyiwa Kaka wa Lissu, Wakili Alute Mughwai Lissu amesema kwamba mara baada ya ndugu yake kutolewa nje na kukaa kwa takribani dakika 30 siyo yeye Lissu peke yake aliyefurahi bali ndugu wote waliokuwepo hospitalini hapo walifurahia mno hilo tukio.


Bw. Alute amesema kwamba awali Manesi walipanga kumtoa nje Jumamosi (Oktoba 14) na kwa kuwa Lissu alijua tunakwenda, aliwaeleza wasimtoe bali wasubiri ndugu zake wafike.


"Nilikuwa mimi na ndugu wengine. Ilipofika saa 10 jioni tulimtoa na mimi ndiye nilimtoa ICU, alifurahi na sisi tulifurahi kwa hatua hiyo,” amesema Kaka huyo mkubwa wa Lissu.


Alute ameeleza kwamba baada ya Lissu kupata upepo wa nje kwa nusu saa nzima alirudishwa wodini ambako amefafanua siyo ICU tena ingawa pia kuna ulinzi na uangalizi wa karibu na si kila mtu anaweza kumwona na kuongeza kwamba hali ya ndugu yake inazidi kuimarika huku akili zake zikiwa timamu.


Pamoja na hayo Alute amesema kwamba suala la kumpeleka sehemu tofauti ya matibabu ndugu yao familia ndiyo itakayoshughulika zaidi kwa ukaribu na kuongeza kwamba, ndugu wengine wapo sehemu mbalimbali kama Kenya, Australia, Marekani, Canada ambao watabidi wajadiliane kwanza ndipo watatoa taarifa juu ya nini kinaendelea.like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI
No comments:

Post a Comment