SENETA JEFF FLAKE AJIUZULU KWA KUMKOSOA TRUMP - EDUSPORTSTZ | Habari za Ajira, Mapenzi, Michezo, Elimu, Kilimo, Technology, Siasa na Mziki,

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Wednesday, 25 October 2017

SENETA JEFF FLAKE AJIUZULU KWA KUMKOSOA TRUMP
Seneta wa Chama cha Republican nchini Marekani, Jeff Flake, amesema hatogombea nafasi yake katika uchaguzi wa mwaka 2018.

Amesema nafasi yake inaweza isiwepo katika chama hicho.

Katika hotuba kali inayokosoa utawala wa rais Trump, seneta huyo wa jimbo la Arizona amesema katu hatoacha kusema.

Ameongeza kusema kuwa siasa za Marekani zimekuwa za kutojali, na tabia ya kujishusha hadhi kutoka ikulu ya Marekani.


Lakini amesema, desturi ya kudharau maadili ya demokrasia na misingi yake katu isionekane kama jambo la kawaida.


Mwanzoni, rais Trump alilaumiwa na seneta mwengine wa Republican, Bob Corker, ambae alimweleza rais huyo kama rais ambae sio mwaminifu.


Msemaji kutoka ikulu ya White House Sarah Sanders amesema "huenda ni hatua nzuri" Bwana Flake anajiuzulu, akiashiria kwamba hatoshinda kuchaguliwa tena.like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI
No comments:

Post a Comment