POLISI WAMWACHIA SHEIKH PONDA - EDUSPORTSTZ | Habari za Ajira, Mapenzi, Michezo, Elimu, Kilimo, Technology, Siasa na Mziki,

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Sunday, 15 October 2017

POLISI WAMWACHIA SHEIKH PONDA
Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda.

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limemwachia kwa dhamana Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda.

Pondà ameachiwa leo Jumamosi jioni baada ya kushikiliwa na Jeshi hilo tangu jana Ijumaa asubuni akituhimiwa kutoa lugha za kichochezi katika mkutano wake na waandishi wa habari Jumatano iliyopita.

Akizungumza Msemaji wa Jumuiya hiyo, Sheikh Rajabu Katimba amesema: “Sheikh Ponda ameachiwa kwa dhamana na atatakiwa kuripoti tena polisi.”

Awali, Kamanda wa Kanda hiyo, Lazaro Mambosasa alisema kwamba uchunguzi dhidi ya Ponda ulikuwa ukiendelea na kama ungekamilika angepewa dhamana.

“Upelelezi unaendelea na ukikamilika tutaangalia kama atapata dhamana au tutampeleka mahakamani,” alisema Mambosasa kabla ya Sheikh Ponda kuachiwa.

Wakili wa Ponda, Profesa Abdallah Safari amesena: “Ni kweli Sheikh Pondà ameachiwa, ni lini atarudi tena sijajua ila sidhani kama watampeleka mahakamani.


 like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI
No comments:

Post a Comment