MWANASIASA WA UPINZANI AHUKUMIIWA KIFUNGO CHA MIAKA 25 JELA - EDUSPORTSTZ | Habari za Ajira, Mapenzi, Michezo, Elimu, Kilimo, Technology, Siasa na Mziki,

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Tuesday, 31 October 2017

MWANASIASA WA UPINZANI AHUKUMIIWA KIFUNGO CHA MIAKA 25 JELA


Mwanasiasa wa upinzani ahukumiwa miaka 25 jela Cameroon

Shirika la haki za binadamu la Amnesty International limeikosoa mahakama ya kijeshi nchini Cameroon kwa kumhukumu kiongozi mmoja wa upinzani miaka 25 jela kwa makosa ya kuchochea uasi.

Aboubakar Siddiki - kiongozi wa chama cha upinzani kaskazini mwa nchi, ndiye mwanasiasa aliyepelekwa jela katika harakati za Cameroon za kuuzima upinzani hivi karibuni.

Hakuna ushahidi uliotolewa mahakamani kuchangia hukumu kama hiyo , taarifa ya Amnesty International ilisema.
Ulinzi waimarishwa Cameroon
Majeshi ya Cameroon tuhumani

Alikamatwa mwaka 2014 baada ya kulaumiwa kwa kupanga kuipindua serikali ya Rais Paul Biya.

Bwana Biya amekuwa madarakani tangu mwaka 1982 na wakosoaji wake wanamtaja kuwa dikteta.

Watu kadhaa wameuawa na mamia kukamatwa wakati wa maandamano katika eneo hilo lenye watu wanaozungumza lugha ya Kiingereza na ambao wanalalamika kutengwa.


like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>



CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI








No comments:

Post a Comment