MWAKIBINGA: ZITTO NI KAMA HARMORAPA - EDUSPORTSTZ

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Monday, 30 October 2017

MWAKIBINGA: ZITTO NI KAMA HARMORAPA


O

Kijana kutoka kundi la Vijana Wazalendo nchini , James Mwakibinga akizungumza na Waandishi wa Habari Kumpinga Mbunge wa Kigoma mjini Zitto Zuberi Kabwe juu ya taharif anazotoa kw akupinga juhudi za Rais John Pombe Magufuli katika kupambana wizi wa Rasilimali za umma nchini.


Waandishi wa Habari walishiriki mkutano wa James Mwakibinga akzungumza kumpinga zito juu ya matamshi yake anayotoa kwa serikali ya Chama Cha Mapinduzi.KIJANA kutoka Kundi la Vijana Wazalendo nchini, James Mwakibinga, amekuja juu na kumshukia kiongozi wa Chama cha Act- Wazalendo, Zitto Kabwe na kusema anatafuta kiki kama Harmorapa kwa kupingana na kasi ya Rais Dk .John Pombe Magufuli katika vita dhidi ya ufisadi uliofanyika katika madini nchini.


Mwakibinga amesema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari na kuwaeleza kuwa mambo yanayofanywa na kiongozi huyo siyo ya kizalendo na hayafai kufumbiwa macho na mtu yoyote mwenye akili na mwenye dhamira ya kweli kwenye taifa lake.“Nadiliki kusema kuwa game changer amebadilisha mchezo hivyo wanasiasa wanashindwa kufanya kazi katika majimbo yao na kazi yao imekuwa kufanya upotoshaji juu ya kazi zilizofanywa na Rais Dk John Pombe Magufuli hasa katika swala zima la kuokoa mali za Watanzania katika sekta ya madini,” amesema Mwakibinga.Amesema Zito anatakiwa kufanya siasa za kistaarabu na kuacha kupayuka tu kwani hii ni miaka miwili bado mitatu hivyo zama hizi zimebadilika hakuna utaratibu tena wa mashirika kuwahonga viongozi wa kisiasa.Mwakibinga amesema kuwa vijana wazalendo wako nyuma yake watamlinda na kusimamia misingi yote ya kulinda rasilimali za wananchi zisiendelee kuibwa.

 like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI
No comments:

Post a Comment