MTIHANI WA KIDATO CHA NNE KUANZA KESHO TAREHE 30.10.2017 - EDUSPORTSTZ

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Sunday, 29 October 2017

MTIHANI WA KIDATO CHA NNE KUANZA KESHO TAREHE 30.10.2017


Kidato cha Nne Kuanza Mtihani ya Taifa Kesho


Mitihani ya Taifa kidato cha nne hapa nchini inatarajiwa kufanyika siku ya kesho nchi nzima ambapo watahiniwa 385,938 wanatarajiwa kufanya nchini.

Hyo yamesemwa leo, Oktoba 29,2017 na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta), Dk Charles Msonde .

Dk Msonde amesema mtihani huo utaanza kesho Oktoba 30,2017 hadi Novemba 17,2017 huku maandalizi ya mitihani yameshakamilika.

Amezitaka kamati za mitihani za mikoa na halmashauri kuhakikisha utaratibu wa uendeshaji wa mitihani unafuatwa.

Katibu mtendaji huyo amewataka wanafunzi kuacha vitendo vya udanganyifu wakati wa kufanya mitihani kwa kuwa wanaweza kufaulu bila kufanya hivyo.

Dk Msonde ametoa onyo kwa wasimamizi na wanafunzi watakaojihusisha na udanganyifu na kusema kuwa baraza hilo halitasita kuwafutia mitihani wote.

.....EDUSPORTSTZ INAWATAKIA WATAHINIWA WOTE MITIHANI MYEMA ......


 like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI
No comments:

Post a Comment