MKE WA DR SLAA ATAJWA KWENYE KESI YA LULU - EDUSPORTSTZ | Habari za Ajira, Mapenzi, Michezo, Elimu, Kilimo, Technology, Siasa na Mziki,

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Tuesday, 24 October 2017

MKE WA DR SLAA ATAJWA KWENYE KESI YA LULU


Mke wa Dkt Slaa Atajwa Kesi Kwenye Kesi Inayomkabili Lulu ya Kumuua Kanumba Bila Kukusudia

Kesi ya kuua bila kukusudia inayomkabili muigizaji wa filamu bongo Elizabeth Michael, (Lulu) imeendelea leo katika mahakama kuu jijini Dar es salaam, ambapo upande wa utetezi umeshindwa kuendelea kutoa ushahidi wake kwa kukosekana shahidi mwingine.

Shahidi huyo aliyetajwa kuwa ni mke wa aliyekuwa katibu mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilbroad Slaa, Bi. Jacqueline Mushumbusi ambaye yuko nje ya nchi, ushahidi wake umekataliwa kupokelewa na mahakama mpaka awepo mwenyewe au askari ambaye aliandika maelezo yake afike mahakamani kutoa ushahidi huo.

Hapo jana wakili wa mshtakiwa Peter Kibatala aliiomba mahakama iruhusu kupokelewa kwa ushahidi utakaotumwa na Bi. Mushumbusi, lakini mahakama imekataa ombi hilo ikisema upande wa utetezi hauwezi kusoma ushahidi huo na kutoa uamuzi wake wa kutaka shahidi awepo mwenyewe au askari aliyeandika ushahidi huo.
Kesi hiyo imeghailishwa mpaka kesho Oktoba 25, ambapo inatarajiwa askari aliyeandika ushahidi wa Bi. Jacquline Mushumbusi, kuwasili mahakamani hapo na kutoa ushahidi wake.

like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI
No comments:

Post a Comment